MICHONGO KAMILI

Sunday, 18 January 2015

TANGAZO LA MITIHANI KIDATO CHA NNE 2015

Ikiwa ni bado matokeo ya kidato cha nne 2014 hayajatangazwa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la
Tanzania (NECTA), Dk. Charles Msonde.Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato Cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) Mwezi Novemba 2015 kwamba usajili umeanza rasmi tarehe 01 Januari 2015.
Watahiniwa watakaojisajili katika kipindi cha kawaida yaani tarehe 01 Januari 2015 hadi 28 Februari 2015 watalipa ada ya Shilingi 50,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 30,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Maarifa (QT).
Watahiniwa watakaojisajili kwa kuchelewa yaani kuanzia tarehe 01 Machi 2015 hadi tarehe 31 Machi 2015 watalipa ada ya Shilingi 65,000/ kwa Kidato cha Nne na ada ya Shilingi 40,000/- kwa mtihani wa Maarifa (ada pamoja na faini).
 Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani: www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo wanavyokusudia kufanyia mtihani kuchukua namba rejea (Reference Number). Wakuu wote wa vituo nchini wamekabidhiwa namba rejea na watazigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo. Aidha waombaji watapaswa pia kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au M-Pesa kabla ya kujisajili kwani hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kulipa ada ya mtihani. Waombaji wote wazingatie kwamba kipindi cha usajili kitafungwa rasmi tarehe 31 Machi 2015
Imetolewa Na: KATIBU MTENDAJI

SOURCE- TANZANIATODAY.CO.TZ

Saturday, 17 January 2015

BREAKING NEWS: MATOKEO YA FORM TWO HAYA HAPA

"BOFYA HAPA KWA MATOKEO YA SHULE YOYOTE UITAKAYO

TANZANIA NZIMA"

 

BOFYA MAJINA KWA BAADHI YA SHULE HIZI HAPO CHINI

1.  MATOKEO YA UGOMBOLWA

2.MATOKEO YA MADIBA

3. MATOKEO YA TUSIIME

4.MATOKEO YA KINYEREZI 

5.MATOKEO YA ZAWADI

6.MATOKEO YA LIWALE 

7.MATOKEO MIGOMBANI 

8.MATOKEO YA MAGOZA

9. MATOKEO BUZA SEC

 

MCHANGANUO  ULIOTUMIKA KATIKA MATOKEO HAYA

 1.    EXTINCTION  (DIV 1) =  FIRST CLASS  (UFAULU WA JUU)

2.     MERIT  (DIV 2)             =  UPPER SECOND CLASS (UFAULU MZURI)

3.    CREDIT  (DIV 3)            =   SECOND CLASS (UAULU WA WASTANI)

4.    PASS    (DIV 4)                =  LOWER SECOND (UFAULU WA KAWAIDA)

5. FAILURE   (ZERO 0 )       = AMEFELI 

Tuesday, 23 December 2014

TIBAIJUKA TUPA KULEEEEE.....MUHONGO KIKAANGONI.

 http://www.ippmedia.com/media/picture/large/Tibaijukabomoa(11).jpg

Siku tatu kabla ya skukuu ya christmass......Rais wa Jamhuri wa Tanzania Jakaya Kikwete ametangaza kutengua uteuzi wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka baada ya vyombo vya Serikali kubaini na kijiridhisha kuwa amekiuka maadili ya utumishi wa Umma kwa kuingiziwa fedha kiasi cha Sh1.65bilioni kwenye akaunti yake binafsi.
Rais kikwete ametangaza kufukuzwa kazi kwa Waziri huyo leo alipokuwa anazungumza na wazee wa  mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini hapa, na baada ya kutangaza kufukuzwa kwake maelfu ya wazee waliohudhuria kwenye mkutano huo walipiga kelele za kumpongeza Rais Kikwete kwa uamuzi wake.
Rais kikwete amesema miongoni mwa mapendekezo ya Bunge kuhusiana na sakata la uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Escrow Tegeta yaliyofikishwa kwenye Serikali ni pamoja na kuwajibishwa kwa Bodi ya Shirika la umeme (Tanesco), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Rais Kikwete amesema baada ya uchunguzi wa vyombo husika viliweza kubaini kuwa kiasi cha Sh1.65bilioni kiliingizwa kwenye akaunti binafsi ya Profesa Tibaijuka, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utumishi wa Umma.
“Tumezungumza na Profesa Tibaijuka na tumemuomba atupishe ili tuweze kuteua waziri mwingine kwani viashiri vyote vinaonyesha kuwa alikiuka kanuni na sheria ya maadili ya Umma,” anasema Rais Kikwete.
Aidha Rais Kikwete amesema katika suala la Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter  Muhongo analiweka kiporo maana bado hajapata ufafanuzi kuhusu mambo kadha wa kadha, hivyo pindi atakapopata ufafanuzi na kujiridhisha ataujulisha umma .
Amesema kuhusu suala la bodi ya Tanesco hana shida nalo kwa sababu tayari bodi hiyo imeshamaliza muda wake hivyo ni kama imekwishajifuta yenyewe, na kuongeza kuwa tayari Ikulu imeshapewa taarifa za kumtaka achague bodi nyingine, hivyo ndani ya siku chache bodi mpya ya Tanesco itatangazwa.
Amesema suala la Katibu Mkuu wa Nishati na Madini na viongozi wengine wa utumishi wa Umma ambao wametajwa katika sakata hilo tume ya maadili, Taasisi ya Kuzuia na Kupapambana Rushwa (Takukuru) pamoja na jeshi la polisi wanaendelea kufanya uchunguzi wao, na ikithibitika kuwa walikiuka maadili yao ya kazi sheria stahiki zitachukuliwa.

HABARI KWA NIABA YA GAZETI - MTANZANIA
Breaking News
Loading...

Search This Blog

LIKE PAGE ZETU ZA FACE BOOK

ZINGINE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...