MICHONGO KAMILI

Friday, 14 March 2014

KUPOTEA KWA NDEGE YA MALAYSIA AIR LINE BADO NI KITENDAWILI


Ni takribani siku 7 sasa tangu ndege ya Malaysia air line ipotelee kusiko julikana mara baada ya kutoweka ghafla kwenye rada za vituo vya usimamizi wa  mambo ya anga vya Malaysia, ilipotea wakati ikiwa katika anga hewa la mashariki mwa fukwe za Malaysia au kusini mwa fukwe za china,

 ndege hiyo yenye namba MH370 ilipotea siku ya jumamosi ya tarehe 9 mwezi wa 3 mwaka huu 2014, ilipotea ikiwa na abiria 227 na wafanya kazi 12 kati ya abiria hao, kwa mujibu wa bwana Ronald Kenneth Noble ambaye ni   Interpol Secretary General, inasemekana kuna abiria wawili amabao walikuwa wakisafili ndani ya ndege hiyo kwa kutumia paspoti feki au za kugushi, hii imezua wazo kwa watafiti wa mambo kuwa kuna uwezekano ndege hiyo ikawa imetekwa na magaidi kwaajili ya kuitumia katika shughuri zao za kigaidi, hawa hapa chini ni abiria hao wawili wanao dhaniwa kuhusika na upotevu wa ndege hiyo kama walivyo tajwa na bwana  Ronald Kenneth Noble, japokuwa hakuna mwenye uhakika juu ya hilo hadi sasa.
Ni siku sita sasa tangu kupotea kwa ndege hiyo na serekali  za Malaysia na china zikishirikiana na serekali ya marekani zimekuwa zikifanya jitihada za kutafuta alama yoyote itakayoweza kuwaonyesha wapi ilipo ndege hiyo,

 inasemekana hadi serekali ya Malaysia ikaamua kutumia na waganga wa jadi ambao ni maarufu katika hiyo kama mganga huyu maarufu anaye itwa bwana Ibrahim Mat Zin
Siku mbili baada ya kupotea kwa ndege hiyo ilizuka habari kuwa kuna abiria wa ndege nyingine ameweza kupiga picha usiku kupitia dirishani ikionyesha cheche za moto katika uso wa bahari ya kusini mashariki mwa bara la asia na inawezekana ikawa ni Malaysia airline imedondoka katika usawa wa bahari na kuripuka moto lakini hii nayo ikabaki kuwa moja ya uzushi tu mara baada ya vikosi vya uokoaji kutembelea eneo hilo na kukuta hakuna chochote Zaidi ya meli na boti kadhaa,
Nadharia mbalimbali zinaendelea kutolewa na watu mbalimbali juu ya ilipo ndege hiyo, wengine wanasema inawezekana ikawa ni pembe ya Bermuda ambayo haipo katika ramani ya dunia, Bermuda ni maarufu kwa upotevu wa ndege na meli nyingi Zaidi duniani  pembe tatu hiyo inaundwa na  miji ya  Miami,San juan,PUERTO Rico pamoja na Bermuda yenyewe meli na ndege nyingi zilizopotelea humu zilipotea kwanza kwenye rada za control towers na baadae hazikupatikana hadi leo na hicho ndicho kinachowapa wasiwasi watu wanao isapoti nadharia hii,

 lakini nadharia hii imekosa nguvu baada ya kugundulika kuwa  maeneo hayo ndio maeneo yanayo ongoza duniani kwa kuwa na safari nyingi za majini na angani kwahivyo upoteaji wa vyombo hivyo unaweza kuwa ni kwa bahati mbaya tu! Na hivyo hakuna uhusiano wowote kati ya upoteaji wa ndege hiyo na pembe tatu ya Bermuda.
Nadharia nyingi zimekuwa zikitolewa ikiwemo ya kuvihusisha viumbe kutoka sayari nyingine na upoteaji kwani rada za kijeshi zilinasa kifaa cha umeme kilichosemekana kupita karibu na njia ya ndege hivyo kwa kasi ya kutoweza kunaswa na kamera za rada hizo,lakini hii pia imekosa ushahidi wakutosha .
Pamoja na nadhari zote hizo lakini bado ndege hiyo haijulikani ilipo hivyo wananchi wenye ndugu waliokuwa kwenye ndege hiyo wanamuomba mungu ndege hiyo ipatikane kama inavyoonekana hapa chini maelfu ya waislamu wa Malaysia wakiswali sala ya kuiombea ndege hiyo ipatikane
Na wakati huo huo vikosi vya uokoaji vya Malaysia,China na Marekani vikiendelea kupanua  maeneo ya utafutaji hadi maeneo ya Malacca.

macho ya ndugu hao yamejaa machozi na sura zao ni zenye huzuni kwa asilimia mia moja..


MUNGU SAIDIA KUPATIKANA KWA MH370
MICHONGOKAMILI.BLOGSPOT.COM

No comments:

Post a Comment

0653830825

Breaking News
Loading...

Search This Blog

LIKE PAGE ZETU ZA FACE BOOK

ZINGINE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...