MICHONGO KAMILI

Wednesday, 2 April 2014

TRENI YA MWAKYEMBE INATUTIA MASHAKA!!!!

 

 Ni kama mwaka mmoja na nusu sasa toka treni ya shirika la reli la tanzania (TRL) ianze kufanya safari zake za kusafilisha abiria kupitia maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam, treni hii imekuwa msaada mkubwa kwa watu wanao tokea maeneo yenye idadi kubwa ya wakazi wa jiji hili ambamo treni hiyo imekuwa ikipiga ruti zake za kila siku ukiacha mbagara, kama wewe ni mmoja wa watumia wazuri wa treni hiyo utakuwa umeshuhudia idadi kubwa ya watu wanaotumia usafiri na kupunguza foleni kubwa zilizokuwa zikitokea maeneo ya posta,kariakoo na buguruni


treni hii imekuwa ikikumbwa na matatizo kadhaa ambayo kwa jicho la pili yanaonekana yanazuilika kama ilivyo pata ajari ya kugongwa na roli lenye namba za usajili T 124 ATG   mnamo tarehe 03 October mwaka 2013 lakini tatizo hili lisingewezakutokea kama askari wa barabarani wange tumika maeneo ambayo treni hiyo inapita ikikatiza katika barabara mama za jiji zinazo pitisha magari kwa wingi zaidi kama ile ya buguruni,tabata na ubungo, lakini kikubwa kilicho igusa blog hii hadi kuandika juu ya usafiri huu ni usumbufu uliotokea siku mbili mfululizo kati ya tarehe 1 hadi 2 ya mwezi wa 4 mwaka huu 2014, tarehe 1 mida ya usiku wa saa mbili treni hiyo ilitakiwa imalizie safari yake ya mwisho kutoka stesheni hadi ubungo, abiria wake walikata tiketi kama kawida na kuingia kwenye treni hiyo tayari kwa kysafiri lakini ilipofika saa 2 na dakika kama 20 hivi ilitangazwa kuwa treni hiyo haitoweza kumalizia safari hiyo na abiria wanaombwa radhi kwa usumbufu huo, tatizo kubwa lililotajwa ilikuwa kufeli kwa injini zinazo sukuma gari moshi hilo lakini ilipofika tarehe mbili tena mwandishi wa blog hii alifika katika stesheni hiyo ili kujua kama treni hiyo imeanza safari zake au la! lakini alikuta milango ya ofisi hizo imefungwa na hakuna tangazo lolote lililowekwa kuwataarifu abiria wa usafiri huo ambao jana yake walikatishwa tiketi na hawakurudishiwa pesa zao kwa madhumuni ya kutumia usafiri huo kesho yake yaani tarehe 2 . hivi ni kweli TRL inakosa pesa ya kufanya matengenezo ya injini za treni hizo? kwa mahesabu ya haraka haraka kama kila abiria mmoja analipia shs 400 kwa safari moja na treni ni hiyo kwa kadilio la chini ina uwezo wa kuchukua takribani abiria 1000, hii inaleta jumla ya shs 400000 kwa safari moja tu! chakujiuliza ni  je kwa siku inafanya safari ngapi? na inaingiza shilingi ngapi? na ina muda gani toka ianze! hadi shirika hilo likose pesa ya kufanya marekebisho ya injini hizo?. mi sina mengi yakunena! ni hayo tu!!!
MICHONGOKAMILI.BLOGSPOT.COM

No comments:

Post a Comment

0653830825

Breaking News
Loading...

Search This Blog

LIKE PAGE ZETU ZA FACE BOOK

ZINGINE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...