Serikali ya Tanzania iko hatarini
kukosa dola za Marekani milioni mia saba sawa na trilioni 1.1 kwa fedha za
Tanzania kwa ajili ya mradi wa pili wa mfuko wa changamoto za Milenia (MCC)
kutokana na kushamiri kwa vitendo vya rushwa nchini humo.
mheshimiwa ZITTO KABWE aliye wasilisha mada hiyo bungeni
Marekani imebainisha kuwa mkataba wa
pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC)
utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa
kashfa hiyo.
Haya yanajiri wakati Rais Jakaya
Kikwete akisubiriwa kutoa maamuzi ya mapendekezo yaliyofikiwa na Bunge
kuhusiana na sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka kaunti
ya Tegeta Escrow wiki ijayo.
Katika tamko hilo kwa umma ambalo
limewekwa kwenye tovuti ya MCC, bodi ilieleza kutambua umuhimu wa kusubiri na
kuona utekelezaji kamilifu wa tamko lililotolewa na Ikulu ya Tanzania Desemba
9, mwaka huu kwamba itachukua hatua za haraka na kutoa maamuzi dhahiri na
thabiti kuhusu maazimio ya Bunge juu la suala la IPTL.
Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa
Marekani nchini Tanzania ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC waliokutana katika
mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa na hali ya rushwa
nchini Tanzania.
Uamuzi huo wa Marekani ambayo
inafadhili miradi mingi ya mabilioni ya fedha ni mtihani wa pili kwa Rais
Kikwete baada ya ule wa maazimio ya Bunge yaliyotaka viongozi wakiwamo mawaziri
waliotajwa katika kashfa hiyo kuwajibishwa.
Wanaotakiwa kuwajibishwa na Rais
Kikwete ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo na Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Eliakimu Maswi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji
Frederick Werema.
Novemba mwaka huu, Serikali ya
Marekani kwa kupitia MCC, ilikubali kutoa ruzuku ya hadi Dola za Kimarekani
milioni 9.78 kwa ajili ya maandalizi ya miradi ya uwekezaji yenye matokeo
makubwa katika sekta ya nishati nchini.
Tanzania ilikuwa mojawapo ya nchi
kumi zilizojadiliwa na Bodi ya MCC iliyokutana kuangalia kama nchi hizo
zimekidhi vigezo vya kuendelea na mchakato wa kuandaa mikataba mipya.
Wakati wa mkutano wa 16 na 17 wa
Bunge, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alidokeza
kusudio la Marekani kukataa kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya MCC, lakini
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alikanusha taarifa hizo.
Juhudi za BBC kumtafuta Balozi wa
Marekani nchini Tanzania, Mark Childress,aweze kuzungumzia juu ya ripoti hiyo
ziligonga mwamba kutokana na sababu za kiprotokali .
HABARI HII NI KWA HISANI
YA BBC SWAHILI.COM
HABARI HII NI KWA HISANI
YA BBC SWAHILI.COM
No comments:
Post a Comment
0653830825