Wakati macho na masikio ya Watanzania
wengi kwa siku kadhaa yalielekezwa Dodoma katika mjadala uliokuwa ukihusiana na
suala la wizi wa fedha zaidi ya shilingi bilioni 320 katika akaunti ya Escrow
Tegeta,kwa upande wa burudani nako suala la wasanii kuendelea kulizana katika
kazi zao limeendelea kushika kasi ya ajabu hali ambayo inaweza kusababisha mitafaruku
mikubwa kati yao.
Hivi karibuni msanii chipukizi ajulikanaye kama Alawi
Abdallah akitumia jina la kisanii ambalo ni Decent Boy (A5) akiwa na Joseph Msunyalo almaarufu
kama Jos Joh waliachia singo yao inayojulikana kwa jina la X-Girlfriend ambayo
walidai kwamba wamemshirikisha Steve RNB
na ilisambazwa katika vituo mbalimbali vya redio na blogs mbalimbali
ikiwemo Hassbaby Mapacha ,Funguka Live na Bongo Swaggz lakini katika hali ya
kushangaza kumekuwa na uvumi unaoeleza kuwa Steve RNB amedai kuibiwa ngoma yake
hiyo aliyokuwa ameicha studio ikiwa bado haijakamilika.
Kwa mujibu wa maelezo kutoka katika
chanzo chetu cha habari cha blog flani hapa town kimeeleza kuwa Steve RNB,alidai kwamba ngoma hiyo
alikuwa akiifanya katika studio ya Chief Elia ambayo inapatikana maeneo ya
Sinza na alikuwa ameitunga maalum kwaajili ya mpenzi wake lakini anashanga
kuiisikia kupitia vyombo mbalimbali vya habari huku ikidaiwa kwamba
ameshirikishwa ilhali wimbo huo ni mali yake.
Katika kutaka kuujua ukweli
niliwatafuta Decent Boy naJos Joh ambao wapo mkoani Kilimanjaro kimasomo kwa
sasa walieleza kuwa wimbo huo waliufanya kwa kumshirikisha Steve RNB na hakuna
ukweli wowote kuhusiana na hilo.
“Ukweli ni kwamba wimbo huo tuliufanya
kwa kumshirikisha Steve na wala haukuibwa kama ambavyo watu wengi wamekuwa
wakidai na mimi binafsi nimesikitishwa kusikia hivyo kwani toka nilipoanza
kufanya shughuli zangu za muziki sijawahi kufikiria kufanya hivyo.
Aidha Decent boy ambaye amewahi
kufanya nyimbo kama Stress akiwa na Jos Joh pamoja na Lazima ukae, amesema kuwa
anatarajia kuachia ngoma mpya itakayokwenda kwa jina la “Kilaza” akiwa amemshirikisha
Ali Nipishe, na pia Jos Joh kuachia
wimbo wake unaojulikana kama “Sitokusahau” akimshiriksha mwanadada Ayler ambapo
nyimbo zote zimefanyika katika Studio ya
Kili Records chini ya Producer Rash the Don.
No comments:
Post a Comment
0653830825