MICHONGO KAMILI

Sunday, 15 February 2015

UTARATIBU WA KUTUNUKU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE NA CHA SITA KWA KUTUMIA MFUMO WA GPA

1. Mfumo wa Wastani wa Pointi (Grade Point Average - GPA)

Huonesha wastani wa pointi alizopata mtahiniwa katika masomo aliyofaulu katika mtihani wake.
GPA hutokana na masomo saba (07) aliyofaulu vizuri zaidi mtahiniwa katika Mtihani wa Kidato cha Nne na masomo matatu (3) ya tahasusi katika Mtihani wa Kidato cha Sita. Mtahiniwa aliyefanya masomo pungufu ya 07 kwa CSEE au pungufu ya 03 kwa ACSEE, atafaulu katika kiwango cha “Pass” endapo atapata angalau Gredi D katika masomo mawili au gredi C, B, B+ au A katika somo moja.

Uzito wa Gredi A= 5, B+ = 4, B = 3, C = 2, D = 1, E = 0.5 na F = 0.

Utaanza kutumika kupanga madaraja ya ufaulu katika Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2014 na Kidato cha Sita (ACSEE) 2015.

2. Ukokotoaji wa GPA ya Mtahiniwa
Hufanyika kwa kuchukua jumla ya uzito wa gredi katika masomo saba (07) aliofanya vizuri kwa Mtihani wa Kidato cha Nne na matatu (3) ya tahasusi kwa Mtihani wa Kidato cha Sita na kugawanya kwa idadi ya masomo. Ukokotoaji huo huzingatia kanuni ifuatayo:

GPA =
Jumla ya Uzito wa gredi za masomo
------------------------------------------------
Idadi ya Masomo

Masomo yatakayotumika katika ukokotoaji wa GPA ya mtahiniwa ni yale ambayo amefaulu; yaani amepata Gredi A, B+, B, C au D.

3. Muundo wa Madaraja Kwa Kutumia Mfumo wa GPA
Katika mfumo wa Wastani wa Pointi (GPA) kutakuwa na madaraja manne ambayo ni Distinction, Merit, Credit na Pass.

 ........................................................................................................................................

Daraja la juu la ufaulu ni Distinction na la chini ni Pass kama ilivyoainishwa katika Jedwali lifuatalo:
 

Mfano; Mtihani wa Kidato cha Nne, mtahiniwa aliyepata ufaulu wa Civics (A), History (B+), Geography (B+), Kiswahili (B), English (C), Physics (C), Chemistry (C), Biology (C) na Mathematics (E) atakuwa na jumla ya pointi 22 kwenye masomo saba aliyofanya vizuri.

Idadi hiyo ya pointi ikigawanywa kwa idadi ya masomo saba (07), Mtahiniwa huyu atakuwa na Wastani wa Pointi (GPA) 3.1 na atatunukiwa daraja la Merit. Katika Mtihani wa Kidato cha Sita mtahiniwa aliyepata ufaulu wa Physics (A), Chemistry (B+), Biology (A), Basic Applied Mathematics (D) na General Study (A) atakuwa na jumla ya pointi 14 kwenye masomo ya tahasusi (PCB). Idadi hiyo ya pointi ikigawanywa kwa idadi ya masomo matatu (03), mtahiniwa atakuwa na Wastani wa Pointi (GPA) 4.7 na atatunukiwa daraja la Distinction.

4. Manufaa ya kutumia Mfumo wa Wastani wa Pointi (GPA);
Kuwa na mfumo wa kutunuku matokeo wa aina moja katika ngazi zote za mafunzo kuanzia Elimu ya Msingi hadi Elimu ya Juu;

Matokeo yaliyo katika mfumo wa wastani wa pointi kwenye cheti yatarahisisha kazi ya udahili wa watahiniwa unaofanywa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) katika ngazi za juu za mafunzo na Mfumo wa wastani wa pointi (GPA) ni rahisi kueleweka kwa wadau wa kada mbalimbali kwa sababu hutoa tafsiri yenye kuonesha mtahiniwa aliye na GPA kubwa ndiye aliye na matokeo mazuri kuliko aliye na GPA ndogo.

Maelezo zaidi kuhusu GPA yanapatikana katika tovuti ya Baraza la Mitihani (www.necta.go.tz).
 


Ufaulu Kidato cha Nne 2014 wapanda kwa asilimia 10

Jumla ya Watahiniwa 196,805 sawa na 68.33% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani kidato cha IV mwaka 2014 wamefaulu ikiwa ni ongezeko la 10.08% kulinganisha na mwaka 2013 ambapo wanafunzi 235,227 sawa na 58.25 walifualu.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dkt Charles Msonde
Jumla ya Watahiniwa 196,805 sawa na 68.33% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani kidato cha IV mwaka 2014 wamefaulu ikiwa ni ongezeko la 10.08% kulinganisha na mwaka 2013 ambapo wanafunzi 235227 sawa na 58.25 walifualu.

Akitangaza matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2014 leo jijini Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dkt Charles Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 89,845 sawa na asilimia 66.61 wakati wavulana ni 106,960.

Amesema watahiniwa wa shule waliofaulu ni 167,643 sawa na asilimia 69.76 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 75,950 sawa na asilimia 68.70 na wavulana 91,693 sawa na asilimia 70.67.

Amesema mwaka 2013 watahiniwa 201,152 sawa na asilimia 57.09 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo hivyo ufaulu kwa wanafunzi wa shule umepanda kwa asilimia 12.67 mwaka 2014 ikilinganishwa na mwaka 2013.

Akizungumzia ubora wa ufaulu, Dkt Msonde amesema kuwa jumla ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya Distinction, Merit na Credit ni 73,832 sawa na asilimia 30.72 wakiwemo wasichana 27,991 sawa na asilimia 25.32 na wavulana ni 45,841 sawa na asilimia 35.33.

Watahiniwa waliopata daraja la PASS 93,811 sawa na asilimia 39.04 na waliofeli kwa kupata daraja la FAIL 72,667 sawa na asilimia 30.24.
Kuhusu ufaulu wa masomo, Dkt Msonde amesema kuwa ufaulu katika masomo ya msingi umepanda kwa kati ya asilimia 1.28 na 11.22 ikilinganishwa na mwaka 2013.

Ufaulu wa juu kabisa umekuwa katika somo la Kiswahili ambapo asilimia 69.66 ya watahiniwa wote wamefaulu na ufaulu chini kabisa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 19.58.

Amesema Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 184 baada ya kubainika kufanya udanganyifu, kati yao 128 ni watahiniwa wa kujitegemea na 56 ni watahiniwa wa shule.

Akizitaja shule kumi bora kwa ufaulu


Dkt Msonde amesema shule hizo ni;
Kaizirege mkoa wa Kagera
Mwanza Alliance mkoa wa Mwanza
Marian Boys mkoa wa Pwani
St. Francis Girls mkoa wa Mbeya
Abbey mkoa wa Mtwara
Feza Girls mkoa wa Dar es salaam
Bethel sabs Girls mkoa wa Iringa
Marian Girls mkoa wa Pwani
Feza Boys mkoa wa Dar es laam.

Shule 10 za mwisho ni;
Manolo mkoa wa Tanga
Chokocho mkoa wa Pemba
Kwalugulu mkoa wa Tanga
Relini mkoa wa Dar es salaam
Mashindei mkoa wa Tanga
Njelekela Islamic Seminary mkoa wa Kigoma
Vudee mkoa wa Kilimanjaro
Mnazi mkoa wa Tanga
Ruhembe mkoa wa Morogoro
Magoma mkoa wa Tanga.

Dkt Msonde pia ametaja watahiniwa 10 waliofanya vizuri kuwa ni;
Nyakaho Marungu kutoka Baobab Pwani
Elton Sadock Jacob kutoka Feza Boys Dar es salaam
Samwel M Adam kutoka Marian Boys Pwani
Fainess John Mwakisimba kutoka kutoka St Francis Girls Mbeya
Mugisha Reynold Lukambuzi kutoka Bendel Memorial Kilimanjaro
Paul W Jijimya kutoka Marian Boys Pwani
Angel Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya
Atuganile Cairo Jimmy kutoka Canossa
Jenifa Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya
Mahmoud Dadi Bakili kutoka Feza Boys.
 
Habari kwa hisani ya Jamii forum.com 

No comments:

Post a Comment

0653830825

Breaking News
Loading...

Search This Blog

LIKE PAGE ZETU ZA FACE BOOK

ZINGINE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...