MICHONGO KAMILI

Sunday, 20 October 2013

JULIAS NYAISANGA AFARIKI DUNIA "MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI"   AMIN
 Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari mkoa wa Morogoro,Aziz Msuya Amethibitisha  kwa njia ya simu toka mjini morogoro kuwa mtangazaji mkongwe nchini Tanzania Julius Nyaisanga 'Uncle J" amefariki dunia  leo asubuhi katika hospitali ya Mazimbu iliyoko katika Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) eneo la Mazimbu alikokuwa amelazwa.
Msuya ameeleza kuwa Mwili wa Marehemu utahamishiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro asubuhi hii kwa ajili ya taratibu zingine.
Nyaisanga alikuwa ameshaomba likizo ya mapumziko kutokana na kutoka Radio Aboud ambako alikuwa akifanyakazi kutokana na kuugua



Kwa mujibu wa chanzo chetu taarifa za kifo chake zimezagaa asubuhi hii na bado haijafahamika zaidi sababu za kifo chake



Julius Nyaisanga  alijulikana sana tangu akifanya kazi Redio Tanzania sasa hivi inajulikana kama TBC Taifa,ITV na Redio One stereo kabla ya kwenda Morogoro kujiunga na Radio Aboud.


No comments:

Post a Comment

0653830825

Breaking News
Loading...

Search This Blog

LIKE PAGE ZETU ZA FACE BOOK

ZINGINE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...