Kutiwa
saini kwa makubaliano hayo ni hatua muhimu ya kukuza mshikamano wa jumuiya hiyo
yenye nchi tano.
Makubaliano hayo ya kisheria yalitiwa saini na viongozi
wote watano wa jumuiya ya afrika mashariki kwenye kongamano la 15 lenye maudhui
ya kuwa na sarafu moja.
Akizungumza kwenye kongamano hilo katibu mkuu wa jumuiya
ya Afrika mashariki bwana Richard Sezibera anasema kubuniwa kwa mkataba wa kuwa
na sarafu moja ni hatua muhimu ya mshikamano haswa baada ya kuwa na soko la
pamoja na umoja wa forodhani ambazo zinasaidia usafirishaji wa bidhaa na
mitaji.
"Eneo letu linapiga hatua kubwa ya mshikamano haswa
baada ya kutiwa saini kwa makubaliano ya kuwa na sarafu moja. Umoja huu wa
sarafu unaiweka jumuiya yetu kwenye awamu nyingine na ni hatua muhimu. Kutiwa
saini kwa makubaliano Haya pia ni mwamko mpya wa mshikamanno wa kifedha."
Kutiwa saini kwa sheria hii ya sarafu moja kunatoa
nafasi kwa nchi wanachama kuanza kuondoa sarafu zao za ndani ya nchi ili
baadaye kuanza kutumia sarafu ya pamoja kote kwenye jumuiya ya afrika
mashariki.
Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo ambaye ni Rais wa Kenya
Uhuru Kenyatta anaiona hii kama hatua muhimu ambayo itavutia zaidi wawekezaji
kwenye eneo la afrika mashariki.
"Wafanyi biashara watapata Uhuru zaidi wakufanya
shughuli zao huku nao wawekeaji wakiongezeka wakipata fursa bora ya kuja kwenye
kanda hii. Tukiwa na manufaa kama hayo bila shaka uwekezaji utaongezeka na
kuboresha uchumi wetu"
Chini yasheria hii nchi wanachama wa EAC wanatakiwa
kuwasilisha sera zao za kubadilisha fedha kwenye benki kuu ya afrika mashariki
itakayobuniwa, hii ikiwa ni hatua za kuelekea kuwa na sarafu ya pamoja.
Wajibu wa benki hiyo kuu ya afrika mashariki itakuwa ni
kuthibiti dhamani ya sarafu moja na pia kusimamia maswala yote ya kifedha
kwenye kanda.
Lakini ingawa viongozi wa afrika mashariki wanaisifu
hatua hii ya sarafu moja na kuitaja kuwa yenye manufaa kwa mshikamano, wataalam
wanahoji kwamba bado kuna maswala muhimu kuliko kuwa na umoja wa sarafu kama
vile biashara baina ya nchi wanachama.
Bwana Louis Kasekende ni naibu gavana wa benki kuu ya
Uganda.
"Sitaki tuzingatie kupita kiasi kuwa na sarafu ya
pamoja. Lazima pia tuzingatie mambo ambayo tungependa kufanikishsa Kama vile
maswala ya maendeleo ya kiuchumi. Tunahitaji kufanya biashara zaidi kwa kuuza
bidhaa na huduma miongoni mwetu."
Lakini Gavana wa benki kuu ya Tanzania Profesa Benno
Ndulu ana maoni tofauti.
"Tutakuwa tu na sarafi moja kwa hiyo inarahisisha
sana biashara na inarahisisha pia kuwa na soko moja kubwa"
Tayari jumuiya ya afrika mashriki imefanikiwa kubuni
soko la pamoja na umoja wa forodha hali ambayo imeimarisha biashara kufuatia
kuondolewa kwa vikwazo vya barabarani na pia mipakani.
Nchi zote tano zina zaidi ya watu million 135 na kwa
pamoja zina pato la jumla la dola bilioni 85.
Mkataba huu wa sarafu moja uliotiwa saini leo
utatekelezwa ndani ya miaka kumi na hapo ndipo jumuiya ya afrika mashariki
itaanza kutumia pesa moja tu.
No comments:
Post a Comment
0653830825