NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KUTUMIA SARAFU MOJA BAADA YA MIAKA 10
Naibu Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayeshughulikia Miundombinu,Dk Enos Bukuku akizungumza na
waandishi wa habari jijini Kampala leo juu ya hatua zilizofikiwa katika
kuweka saini Itifaki ya Sarafu Moja jumamosi wiki kwenye Uwanja wa Kololo
nchini Uganda,kushoto ni Mkufunzi na Mwandishi Mkongwe,Jenerali Ulimwengu.
Na Mwandishi Wetu,Kampala
Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jumamosi wiki
wameweka saini Itifaki ya Sarafi Moja ikayowezesha matumizi ya Sarafu moja
katika nchi hizo.
Matumizi ya Sarafu moja yatachukua muda kutekelezwa ili kutoa nafasi ya
utekelezaji wa michakato mbalimbali ya kuoainisha sera na sheria ikiwa ni
pamoja na kuanzishwa kwa taasisi kadhaa kabla ya kuanza kutumika Sarafu hiyo
inaweza kuchukua miaka 10.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ,Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayehusika
na Miundombinu,Dk Enos Bukuku amesema utaratibu huo utazifanya nchi wanachama
kukubaliana katika mambo ya sera za fedha za Jumuiya hiyo na kuwa na Benki
Kuu ya EAC.
Amesema wataalamu katika Sekretariat ya Jumuiya hiyo wamekua wakienda
kujifunza mfumo wa utendaji kazi wa Sarafu moja kwenye nchi za Umoja wa
Ulaya(EU).
Naibu Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayeshughulikia Miundombinu,Dk Enos Bukuku akizungumza na
waandishi wa habari jijini Kampala leo juu ya hatua zilizofikiwa katika
kuweka saini Itifaki ya Sarafu Moja jumamosi wiki kwenye Uwanja wa Kololo
nchini Uganda,kushoto ni Mkufunzi na Mwandishi Mkongwe,Jenerali Ulimwengu.
Na Mwandishi Wetu,Kampala Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jumamosi wiki wameweka saini Itifaki ya Sarafi Moja ikayowezesha matumizi ya Sarafu moja katika nchi hizo. Matumizi ya Sarafu moja yatachukua muda kutekelezwa ili kutoa nafasi ya utekelezaji wa michakato mbalimbali ya kuoainisha sera na sheria ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa taasisi kadhaa kabla ya kuanza kutumika Sarafu hiyo inaweza kuchukua miaka 10. Akizungumza na waandishi wa habari leo ,Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayehusika na Miundombinu,Dk Enos Bukuku amesema utaratibu huo utazifanya nchi wanachama kukubaliana katika mambo ya sera za fedha za Jumuiya hiyo na kuwa na Benki Kuu ya EAC. Amesema wataalamu katika Sekretariat ya Jumuiya hiyo wamekua wakienda kujifunza mfumo wa utendaji kazi wa Sarafu moja kwenye nchi za Umoja wa Ulaya(EU). |
No comments:
Post a Comment
0653830825