MICHONGO KAMILI

Wednesday, 19 February 2014

"HIVI SASA NI WAKATI WA KUTENGENEZA IMAGE YA JERUSALEM PEKEE".................... ASEMA JACOB STEVEN

YULE MKALI WA SHKAMOO MZEE NA NYINGINE NYIIINGI YAANI "JB" JACOB STEVENANAKUJA NA CHUMA KINGINE "WAGENI WANGU"

TRAILLER YA WAGENI WANGU

Utakapozungumzia watengenezaji wazuri wa
filamu za Kitanzania huwezi kuacha kuwataja Jerusalem
Film ambayo kampuni hii ipo chini yake Bonge la Bwana “JACOB STEVEN” ambaye pia
katika waigizaji wanaofanya poa sana
hivi sasa katika soko la filamu ndani na nje ya nchi pia huwezi kuacha

kumuorodhesha huyu jamaa.

JB KATIKA POUZI
Juzi kati tulipata fursa ya kuzungumza
nae na tukataka kufahamu mengi sana kutoka kwake
lakini pia kutokea Jerusalem Film akiwa kama mzungumzaji mkuu wa Kampuni hiyo. Na kitu cha mwanzo
kabisa tulichotaka kufahamu ni kuhusiana na suala zima la Jerusalem kutoa
filamu ambazo JB hatujamuona humo ndani hata scene moja, jambo ambalo
limewaumiza vichwa mashabiki wake wengi katika filamu iliyokwenda kwa jina la
BADO NATAFUTA.
alikuwa na haya yakusema;
“Yeah ni kweli, ila lengo la kufanya
hivyo ni kutaka kutengeneza image ya kampuni ya Jerusalem
Film na si lazima ya JB, kwa maana ya kuwa watu wawe na hamu ya kutazama filamu
za Jerusalem. Na
huo naweza nikasema ndiyo mpango wa hivi sasa kwa maana ya kuwa kutakuwa na
filamu za aina mbili ambazo nitakuwa sishiriki na zile ambazo nitakuwa
nashiriki”.
OFFICIAL COVER YA MOVIE AMBAYO IMEFANYA POA SANA 2013 "BADO NATAFUTA"
Lakini jambo jengine ambalo JB
alilizungumzia ni kwamba anawashukuru sana mashabiki wake kwani filamu hiyo ya
BADO NATAFUTA imekuwa filamu ambayo imefanya vizuri sana mwaka jana.Ila bado
tukawa na maswali kwa JB kuwa kwanini ameamua kuhamia katika kutengeneza image

ya Kampuni tu na si JB kama JB?
 
Bi Staa kama anavyojulikana na wengi....
“Hapana, ila unajua jambo muhimu ambalo
tumelilenga hapo ni kuwafanya mashabiki wakishakuwa na imani na Jerusalem ijapo
kuwa JB hayumo ndani ya filamu hiyo itasaidia sana pale ambapo nitakuwa siigizi
tena kutokana na sababu mbalimbali huwenda nimeamua kupumzika, au kwa sababu
nyengine yeyote ile. Hivyo watu bado watakuwa na imani na vitu vinavyozalishwa
na Jerusalem.”
GABO AKIWA KAZINI
Na jambo jengine ni kuhusiana na
mipangilio ya Jerusalem kwa mwaka huu 2014, maana tayari ni mwezi wa pili huu
hivi sasa tunaelekea na hatujaona wala kusikia kazi yeyote mpya kutokea kwako.
Suala ambalo alinieleza kuwa wapo vyumbani wakikamilisha mapishi ya kazi mpya nyiingi
tu ambazo soon zitakuwa sokoni.
GABO AKIWA KAZINI ALIYEKUWA MAIN CHARACTER NDANI YA BADO NATAFUTA
“Kwa filamu ambzo mimi sishiriki mwaka
huu tutakuwa na filamu itakayoitwa WAGENI WANGU ambayo ameshiriki Bi
Hindu,Mhogo Mchungu,Bi Star, na  mzee
mwingine wa Mombasa ambayo hii itatoka recently, halafu tutakuwa na POLICE LOCK
UP ambayo atakuwepo Ben Kinyaiya,Brigit (ambaye ameigiza kama Regina) na Adam
Kuambiana, then tutakuwa na filamu nyingine inaitwa  CHA USIKU ambayo wameshiriki Mayasa Mrisho,
Hemed Suleiman,Cathy Rupia, Shamsa Ford, Brigity na Baba wa Hisia “Haji Adam.
Ila kwa upande wa movie ambazo nashiriki ya kwanza kabisa itakuwa ni HUKUMU YA
NDOA YANGU ambayo nimecheza na muigizaji wa siku nyingi sana Chiki Mchoma,
Mayasa Mrisho, Shamsa Ford, Bi Mwenda, Q Chief, Brigity na Will Sanga. Ambapo
nafikiri movie hii itatoka mwezi wa tatu ama nne”
 
Katika malengo mazuri kabisa ya JB kwa
kutengeneza image ya kampuni yake ni pamoja na suala zima la kuwapa nafasi  au kuwafungulia milango waigizaji mbalimbali
wadogo ili kuwapa nafasi na kuwa waigizaji wakubwa na waigizaji wapende kuigiza
Jerusalem
either JB yupo ama hayupo. Sasa suali langu lilikuja likiuliza kuwa je ni
kuibua  vipaji au vipi maana kama ni kuibua vipaji hatujaona katika mfululizo huo
alionitajia jina ambalo ni jipya katika masikio yetu lakini pia hata katika

movie ya Bado Natafuta halikadhalika.
GABO KATIKA POUZI
“Swali zuri sana, Jerualem haibui vipaji
ila ni inaendeleza vipaji maana kuibua vipaji ni risk. Maana wapo waigizaji
waliokwisha anza kuigiza na wana vipaji, hivyo sera yetu ni kuwapa nafasi

waigizaji hao na kuwafanya wawe waigizaji wakubwa kwa kuwapa movie nyingi.”
JB AKIFURAHIA KAZI NZURI WALIYOIFANYA ZANZIBAR BAADA YA KUTWAA KITU HICHO (KOMBE0
Baada ya maongezi mengi sana na Bonge la Bwana “JB” kupitia 92.5 Hits
fm radio ikishirikiana na Www.ridhiwanshariff.blogspot.com,
kabla ya kumpa nafasi ya kuzungumza na fans wake ikanibidi na mie nimpatie

hongera yake kwa movie ya BADO NATAFUTA kwani hata mie imenivutia.
JB KATIKA POUZI YA PICHA NA JEZI YA TANZANIA
“Thanks bro, Nawaahidi kuwa movie ambazo
tumezitengeneza mwaka huu 2014 watazipenda sana maana waigizaji hawa waliocheza nimekaa
nao kwa muda mrefu tumefundishana, tumeelekezana na kila mmoja ameonesha ana
uwezo mkubwa. Hivyo nawaahidi kwamba hata movie ambazo sitashiriki watazipenda
sana kama ambazo nimeshiriki na mfano wameshaanza kuona kwa BADO NATAFUTA ni
filamu ambayo imefanya vizuri sana na hata zile ambazo nimeshiriki zingine

hazikupendwa sana kama hii ambayo sijashiriki”.


KUPITIA HAPA
HAPA Www.Michongokamili.com UTAWEZA KUSIKIA INTERVIEW YA
JACOB STEVEN NA RIDHIONE SHARIF WA ZANZIBAR
JACOB NA IRENE  KAZINI

No comments:

Post a Comment

0653830825

Breaking News
Loading...

Search This Blog

LIKE PAGE ZETU ZA FACE BOOK

ZINGINE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...