TOP
C KATIKA POUZI
|
Yule mshkaji ambaye
alijitahidi kufanya poa sana katika Industry ya Bongo Fleva kwa hits songs zake
kadhaa ikiwemo "Sababu ya Ulofa" na nyinginezo zikiwa zime recordiwa
ndani ya Sharobaro Records chini yake Raisi wa Masharobaro Bob Juniour.
Nadhani kwa intro hiyo si mgeni saaana katika masikio na
macho ya mafuns wa Bongo Fleva a.
He is Top C ambaye kiukweli alipotea muda
mrefu sana katika gemu na kufikia hata kusababisha kuwepo kwa uvumi wa kuwa
jamaa alibahatisha!!! au ndo keshapigwa chini??? na vitu kama hizo
nini..............!!!
TOP
C
|
Ila juzi kati Top c alifunguka na kuuzima ukimya
wote uliokuwepo dhidi yake na kukanusha suala la kushushwa kimziki na aliyekuwa
bosi wake wa zamani (Babuu Kisouji) alipokuwa chini ya Babuu Entertainment na
Top C kusema kuwa.
"hapana hilo suala si
la kweli, ila tu unajua sisi ni binadamu tunakosea na tunakwazana vilevile.
Kuna mambo tu ya kibinadamu yaliyotokea kati yangu na bosi wangu wa zamani
Babuu Kisouji na hivyo hatukufikia mwisho mzuri ndiyo maana tukaamua kila mmoja
afanye shughuli zake. Ila si kweli kwamba yeye ndiyo kanishusha au kanizuia
nisitoe nyimbo mpya"
Lakini pia Top C alinieleza
kuwa alikuwa na baadhi ya mambo ya kifamilia na nini ndiyo maana akawa kimya,
ila hivi sasa ameshajipanga vizuri na kazi yake mpya ipo tayari na hivi
karibuni tyu itaanza kusikika kwenye
radio stations mbalimbali.
TOP
C NA MAANDALIZI YA KITU KIPYA YAKO HIVIIIIIIIIIIIII
|
"Kuna baadhi ya vityu
tyu vinamaliziwa na muda mfupi tyu itaanza kusikika katika redio stations
mbalimbali. Sijajua ni lini hasaa itakuwa kwa hewa kutokana na hayo ni masuala
ya management yangu ambayo hivi sasa inanisimamia kazi zangu kutokea kule Kenya
"Canden Kane " Ila ikishakuwa tayari tyu nitaitambulisha"
Na zaidi ya hayo Top C
anawaomba mashabiki wake mumpokee vizuri na mumpe support ya kutosha.
No comments:
Post a Comment
0653830825