HATIMAYE Shirikisho la
Soka Duniani, FIFA limemuidhinisha mshambuliaji nyota wa kimataifa wa
Uganda, Emmanuel Okwi kuichezea klabu ya Yanga. Kwa mujibu maelezo wa
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini, TFF, Celesine Mwesigwa
amethibitisha kuwa tayari wameshapokea barua kutoka FIFA ikiwahabalisha
kuwa mchezaji huyo ni halali kukipiga Yanga. Mwesingwa amesema suala
Okwi tayari limeshamalizika ila hawezi kulizungumzia zaidi kwasababu
watatuma taarifa kwa vyombo vya habari kwa ufafanuzi zaidi. Januari 22
mwaka huu ikiwa ni siku mbili tu kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya TFF ilisimamisha usajili wa Okwi kuitumikia Yanga ili
kwanza upatikane ufafanuzi kutoka FIFA juu ya uhalali wake kucheza timu
hiyo. Kamati hiyo ilifikia iliamua hivyo kwasababu ya mgogoro wa
mchezaji huyo na klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia ambapo kulikuwa na
taarifa kuwa alipewa kibali cha muda kuichezea SC Villa ya nchini kwao
ili kulinda kiwango chake.
No comments:
Post a Comment
0653830825