MICHONGO KAMILI

Friday, 21 February 2014

TRAILLER YA PRINCE WILLTH
Yule mkali anaetikisa Tasnia nzima ya Bongo Movie ambae ameweza kuwapiku wakali wengine katika
Tasnia hiyo ya Movie kwa hapa nyumbani Tanzania na baadhi tu ya Filamu zake
ambazo ameshaziachia kama vile BOXEERA, EDA, RAMADHANI KAREEM, na kuweza
kufanya poa sana katika soko la hapa nyumbani na hata kimataifa pia.Na si
mwingine bali namzungumzia Ussi Hajji almaaruf kama “FEY au FEYSAL”

Mkali huyo ambaye makao makuu yake kikazi na hata
kifamilia yakiwa visiwani Zanzibar akiwa chini ya kampuni yake inayofahamika
kama Zan Effects. hivi juzi kati bllog hii ilipata fursa ya kuzungumza nae in an
Exclusive Interview iliyo endeshwa na mmoj wa waandishi wa blog hii mr.Ridhione kupitia Hits fm radio 92.5

Lakini mwanzo kabisa tulitaka kufahamu kuhusiana na
lile kosa aliloweza kulifanya katika filamu yake ya mwisho iliyoko sokoni mpaka
hivi sasa “BOXEERA”, pale ambapo alikuwa ndani ya chumba na yeye akicheza kama
verry sensitive Person “mtu mwenye hisia/machache  sana” lakini yule jamaa aliingia mule ndani
na kuchukua kitabu pasi na yeye kugundua chochote kile. Alifunguka kwa kusema
“Sisi ni wanadamu na hakuna mwanadamu mkamilifu,
tumezipokea comment za watu vizuri na tumeahidi kuzifanyia kazi kwa sababu watu
wengi sana walinipigia simu na kunambia kuwa inakuwaje wewe kama jini halaf
mtu anakuja na wewe hujahisi hata chochote?? Ni jamabo ambalo haliwezekani
kabisa. Ila ilikuwa ngumu tu kurudi tena location kutokana na mambo kadha wa
kadha. Hivyo naweza kusema kuwa tutajitahidi kuwa makini pia”

Ila alipomuuliza kuhusiana na maandalizi ya Zan
Effects kwa mwaka huu 2014 kuna nini ambacho kinakuja ama nini wanafanya maaana
ni muda mrefu sasa tangu itoke BOXEERA. Alisema kuwa kutokana na ubora wa
kazi zao ambao huambatana na maandalizi mazuri ambayo lazima yachukue muda
kidogo ………

“Ila soon tyu nitaitambulish The Exclusive one ambayo inakwenda kwa jina la PRINCE WILTH ambayo itatoka katika miezi hii hii

ya hapa mwanzoni. Ijapo katika mwaka huu wa 2014 kuna movie nyingi tu kutokea
Zan Effects  ambazo zitatoka ila hiyo
Prince Wilth itakuwa ya mwanzo as an exclusive. Na naweza kusema kuwa hizi ni
movie ambazo zinaleta mapinduzi katika tasnia ya filamu ambapo ndipo kama
tulivyoanza na Boxeera kama walivyoiona. Lakini mi naahidi itakapotoka nahii
Prince Wilth ndipo watakaposaidiki hili”

Jamaa tulipotaka uthibitisho wa hayo mapinduzi kwa
movie hiyo ya Prince Wilth akatutupia kitu cha trailer ya movie hiyo na
kuifanya blog hii kuwa na sababu mia moja za kuandika habari hii yenye ushahi wakutosha.Ila jamaa alimalizia kwa kusema;
“So mi nitaendelea kufanya vitu vitakavyoleta tofauti
katika tasnia ya filamu, na ningeomba sana watu wangu waendelee kuni support
na kazi zangu ili tuweze kufikia pale ambapo tunafikiria kufika.Nawapenda sana
fans wangu wooooooooote” 
huo ndio mchongo kamili kutoka 
www.michongokamili.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

0653830825

Breaking News
Loading...

Search This Blog

LIKE PAGE ZETU ZA FACE BOOK

ZINGINE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...