WhatsApp has suffered an outage just
days after it was bought by Facebook for $19billion (£11.4billion).
hichi ni kichwa cha habari kinachowekwa na mtandao wa REUTERS siku ya tarehe 22 feb 2014
mtandao wa WHATSAPP uliogunduliwa na Brian Acton na Jan Koum back Ulinunuliwa na wamiliki wa FACEBOOK kwa dolla billion 19 kabla hauja leta hitlafu kwa zaidi ya masaa matatu siku ya tarehe 22 feb 2014 ambapo watumiaji wa WHATSAPP walishindwa kutuma na kupokea picha na video pamoja na mtandao huo kushindwa kukonekti na servers wa mtandao huo kama ilivyo andikwa na mtandao wa habari wa REUTERS katika tareha hiyo hiyo. bado haijawekwa wazi ni kwanini bwana Mark Zuckerberg ambaye ni mgunduzi na mmiliki wa mtandao wa kijamii wa FACEBOOK aliamua kununua mtandao wa WHATSAPP kwa bei kubwa ambayo FACEBOOK kamwe haijawahi kuingia gharama kununua mitandao miongine kama-INSTAGRAM kwa dolla billion 1, BRANCH iliyo nunuliwa kwa dolla million 15 na FACE.COM ya israel ilyo nunuliwa kwa dolla million 100 na zingine nyingi kama TAGTILE,SPOOL,SHAREGROOVE
na mingine mingi ipatayo 45
wamiliki wa mtandao wa WHATSAPP waliomba radhi kwa watumiaji wake waliokua wakikadiriwa kufikia milioni 450 duniani kupitia mtandao wa Twitter siku ya juma mosi mida ya saa 7 na dakika 30 mchana mtandao huo uliendelea kusumbua hadi mida ya saa 11 na dakika 48 mchana ambapo WHATSAPP kupitia twitter kwa mara nyingine ikawafahamisha watumiaji wake ambao wana follow kupitia twitter ambao wapo takriban millioni 1 kuwa WHATSAPP sasa iko sawa na wanaweza kuendelea kuitumia kama mwanzo. wataalam kadhaa wamekua wakitoa mawazo yao kuwa inawezekama bwana Mark Zuckerberg ameamua kununua kila mtandao unaoonekana kupata umaarufu na kutaka kuipiku FACEBOOK ili abakie kuwa kinara wa mitandao ya kijamii duniani.....ni hayo tu
MICHONGOKAMILI.BLOGSPOT.COM
No comments:
Post a Comment
0653830825