Jeshi la Polisi nchinikenya katiika mji mkuu
Nairobi leo limewafyetulia gesi ya kutoa machozi wanafunzi wa shule ya
msingi waliokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa ardhi waliyokuwa
wanatumia kama kiwanja cha kuchezea na mmiliki binafsi.
Polisi hao
wakiwa na Mbwa waliwatawanyta wanafunzi hao, baadhi yao wakisemekana
kuwa watoto wenye umri wa miaka sita baada ya kuuangusha ukuta mpya
uliojengwa kati ya shule yao na uwanja huo.
Wanafunzi hao walikuwa
wamerejea shuleni Lang'ata baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa
shule za umma walipopata kiwanja chao kikiwa kimeuzwa na hata kuwekwa
uzio.
Shule hio ina karibu watoto 1,000 walo kati ya umri wa miaka mitatu na kumi na minne na inasimamiwa na baraza la jiji.
Wanafunzi kadhaa walijeruhiwa katika purukushani hilo wakati polisi
walipoingilia kati na kujaribu kuwatawanya wanafunzi hao waliokuwa
wanazua rabsha.
Baadhi yao walipelekewa hospitalini baada ya kupata majeraha madogomadogo.
Baadhi ya wanafunzi hao walikabiliana na polisi wakiwa wamebeba vijiti na kuwanyoshea.
Polisi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa kwa mawe.
Walimu wa shule hio pia waliandamana wakisaidiwa na wanaharakati wa kisiasa.
Haijajulikana ambavyo mtu huyo aliweka uzio katika kiwanja hicho walichokuwa wakitumia wanafunzi kuchezea.
araza la jiji limesema kuwa ardhi hio ni ardhi ya serikali ingawa
halijazungumzia ambavyo ardhi yenyewe iliuzwa ingawa wanaharakati
wanasema kiwanja hicho kimeuzwa kwa tajiri anayepanga kukitumia kwa
ujenzi.
source - BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment
0653830825