Kwa namna moja au nyingine Huenda uukawa ni mwaka wa neema kwa mshambuliaji Mbwana Samatta wa TP
Mazembe kwa kuwa timu nne za Ulaya zimeonyesha nia ya kumchukua.
Habari za chinichini kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje zinachombeza kuwa, timu nne zimeanza mchakato wa kuwania saini ya mkali wa TP Mazembe SAMATTA, kati ya hizo
ambazo ni kutoka katika nchi za Ufaransa na Italia, zimeonyesha nia ya
kufanya kazi na mshambuliaji huyo Mtanzania.
“Kweli tunayajua majina ya timu nne, kumekuwa na mawasiliano kupitia
meneja wake Tanzania pamoja na uongozi wa TP Mazembe,” kilieleza chanzo
kutoka Ufaransa.
“Tusingependa kuanza kueleza kila kilichopo kwa sasa wala kuzitaja timu zenyewe, lakini tunaamini Samatta anaondoka Mazembe msimu huu.” Alisema tajiri wa TP Mazembe Billionea KATUMBI.
Baada ya taarifa hizo, juhudi zilifanywa na baadhi ya social media ili kumpata meneja wake, Jamal Kisongo ambaye alitoa ushirikiano.
“Kweli kuna timu zinamhitaji, kama nilivyokueleza awali Mbwana si mtu wa
kwenda kufanya majaribio, badala yake kujiunga na timu na kuanza kazi.
“Sasa kinachofanyika ni taratibu na nimekuwa na mawasiliano na uongozi
wa TP Mazembe, hivyo vuteni subira kidogo,” alisema Kisongo akionyesha
kujiamini kuhusiana na mchezaji wake huyo.
Samatta yupo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko na amekuwa mchezaji tegemeo wa kikosi cha Mazembe.
Awali ilielezwa, mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi, alikuwa akifanya
juhudi kuhakikisha Samatta anabaki Lubumbashi, DR Congo, lakini Kisongo
amehakikisha anakwenda mbele zaidi ili kupata mafanikio zaidi.
No comments:
Post a Comment
0653830825