Baada kuhusishwa na sakata la wizi wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo ameamua kumuandikia barua Raisi ya kujiuzulu wadhifa wake. "atakuwa kaambiwa tuuu"
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar
es Salaam, Profesa Muhongo ameelezea furaha yake ya kupatikana kwa
maendeleo ya haraka katika wizara yake kwa kipindi chake akisema kuwa
nidhamu na uwajibikaji vilikuwa dira ya maendeleo wizarani hapo. "kujisifu" ,
Profesa Muhongo amekwenda mbali zaidi na kueleza
kuwa anaamini kujiuzuru kwake kutaisaidia Serikali na Bunge kutuliza
malumbano ya Sakata hilo ambalo linazidi kurudisha nyuma maendeleo ya
nchi.
Amesema yeye si mwizi na hawezi kuuza utu wake kwa kupewa rushwa ili kuwakandamiza watanzania. "kweeeli???"
“Nimeamua kujiuzuru kwa dhati kabisa bila
kushinikizwa na mtu yeyeote, inaonekana mimi ndiyo nitamaliza mjadala
huu wa sakata la Escrow, tuna mambo mengi ya kitaifa yanayotakiwa
kujadiliwa lakini watu wamekazana na Escrow, nimemuandikia Rais barua
rasmi ya kujiuzuru wadhifa wangu, amesema Profesa Muhongo. "bora!!"
Amesema pamoja na kujiuzuru anatarajia mapema
kuzungumza na watanzania ili kuwaeleza ukweli wa sakata la Escrow na
kujiuzuru kwake ili kuvunja majungu yanayoendelea kuitesa Tanzania na
watu wake.
Amesema yeye amelelewa katika malezi yenye maadili
mema na kwamba tokea alipomaliza masomo yake aliaswa kutopokea ama
kutotoa rushwa hivyo hawezi akapokea rushwa kwa ajili ya kuutukana utu
wa mtanzania hicho ndicho kinachomgharimu."laaabda"
Source: MWANACHI (Gazeti)
Source: MWANACHI (Gazeti)
No comments:
Post a Comment
0653830825