Rais Jakaya kikwete wa Tanzania ametangaza mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.
Rais amewateua mawaziri wanane wapya pamoja na manaibu watano.Tangazo hilo lilifanywa na katibu katika ikulu ya rais balozi Ombeni Sefue.
Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhfa wa waziri wa nishati na kawi wa Profesa Muhongo ambaye amejiuzulu mapema leo pamoja na wadhfa wa waziri wa ardhi ambao uliwachwa wazi baada ya kupigwa kalamu kwa Anna Tibaijuka.
Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo ilimshinikiza mwanasheria mkuu pia kujiuzulu.Nafasi ya Profesa Muhongo imechukuliwa na aliyekuwa naibu wa waziri wa ardhi, George Simbachawene
Rais Kikwete amewaapisha mawaziri hao wapya hii leo katika tangazo lililorushwa hewani na runinga ya taifa moja kwa moja.
Hii ndio orodha ya mawaziri walioteuliwa
No comments:
Post a Comment
0653830825