MICHONGO KAMILI

Monday, 30 December 2013

NEY WA MITEGO NI FREEMASSON?

 FREEMASSON NA NEY WA MITEGO !!!!!!!
Blog hii kwa mara ya kwanza imeamua kukuletea jambo ambalo limekuwa gumzo sana midomoni mwa watu.......ni kuhusu uwepo wa dini ya kishetani iitwayo freemasson,inasemekana kuwa  uwepo wa dini hii ume kuwa ni wa kificho sana ....lakini kwa ushahidi mbakli mbali inaonyesha kuwa dini hiyo ipo na ina endesha shughuri zake ulimwengu mzima... ushahidi mmoja wapo ni uwepo wa freemasson hall mjini dar es salaam maeneo ya posta ambalo ni hili hapa chini kama lionekanavyo kwenye picha..
inasemekana dini hiyo imekuwa ikiwashawishi wasanii wakubwa ambao ni kioo cha jamii ili kujiunga na dini hiyo ili kuwa poteza mashabiki wa msanii hao, baadhi ya wasanii wamewa wakitajwa kujihusisha na dini hiyo majina kama DIAMOND PLATNUMZ  na  NEY WA MITEGO yamekuwa yakitamkwa sana mitaani huku yakihusishwa sana na dini hiyo huku sababu kubwa ikiwa ni matendo yao,maneno,skendo,na alama tofauti tofauti ambazo wamekuwa wakizionyesha kwenye mausha yao ya muziki,,,,,,,je   kuna  ukweli  wowote? kwa leo  tutaanza  na ushahidi kadhaa uliokusanywa na blog hii kuhusu msanii ney wa mitego....
Ney wa mitego ametokea kuwa nsanii aliye teka sana soko la muziki wa hip hop hivi karibuni lakini amekuwa akipunguza mashabiki kutokana na skendo mbalimbali kama hii inayo onekana hapa chini.

Tukiachana na skendo hizo bado kume kuwa na alama mbali mbali ambazo msdanii huyo amekuw akizionyesha kwenye video zake huku aki tamka maneno ambayo yana mtambulisha yeye kama rafiki wa dini hiyo kwa mfano kwenye nyimbo yake maaru iitwayo "NASEMA NAO" alimetoa sentensi kadhaa ambazo zina dhihirisha uhusika wake katika dini hi yo kwa mfano aliposema "unataka kwenda mbinguni huwezi fika bila mii" swali ni kwamba  yeye ni nani???? pia  mstari mwingine ni ule usemao "mimi ndo rafiki wa lucifer !! utanieleza nini " yeye ni rafiki wa LUCIFER  na lucifer ni mungu wa dini hiyo kama anavyo onekana hapa chini
pia amekuwa akionyesha alama mbali mbali ambazo ni alam,a za dini hiyo kama inavyoonekana hapa chini
hakuishia hapo pia katika video yake iitwayo "NASEMA NAO" ameonyesha alama hizo mara nyingi zaidi na kwakukusudia kabisa kwa mfano katika picha zifuatazo

je hii ni bahati mbaya? au ni swaga kama wasemavyo vijana wa mjini ambao wamekumbwa na mkumbo huo wa kuiga matendo ya wasanii wakubwa huku wakiita swaga!!!!!!! tuendelee!!

je na hii ni bahati mbaya? au bado ni swaga? sijui!!

  hatuhitaji kutumia miwani kuona alama hizi !!
huu ni ushahidi tu uliokusanywa na blog hii na halazimishwi mtu kukubaliana na ushahidi huu....
mhhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!
mwishoni mwa nyimbo hiyo anasema hivi  "I represent my hood" lakini badala ya kuonyeshwa manzese anaonyeshwa akiwa na watu kadhaa ambao wamevaa mavazi ya kufunika ambayo inaaminika kuwa hutumika katika ibada za freemasson je? ana represent manzese au makundi ya watu hao? kilichoonyeshwa ni hiki!!!

haya ni mambo kadhaa tu anayo yafanya msanii huyun  nakufanya wengi waamini juu ya uhusika wake kwa dini hiyo ya FREEMASSON   Lakini vipi kuhusu DIAMOND?
Acha blog hii ikusanywe kwanza kisha itarudi jamvini kuwapasha yaliyomo!!!   ALLEVIDEH!

Tuesday, 3 December 2013

Viongozi wa jumuiya ya afrika mashariki waliokutana mjini Kampla Uganda wametia saini sheria ya makubaliano ya kuwa na sarafu ya pamoja.



Kutiwa saini kwa makubaliano hayo ni hatua muhimu ya kukuza mshikamano wa jumuiya hiyo yenye nchi tano.
Makubaliano hayo ya kisheria yalitiwa saini na viongozi wote watano wa jumuiya ya afrika mashariki kwenye kongamano la 15 lenye maudhui ya kuwa na sarafu moja.
Akizungumza kwenye kongamano hilo katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki bwana Richard Sezibera anasema kubuniwa kwa mkataba wa kuwa na sarafu moja ni hatua muhimu ya mshikamano haswa baada ya kuwa na soko la pamoja na umoja wa forodhani ambazo zinasaidia usafirishaji wa bidhaa na mitaji.
"Eneo letu linapiga hatua kubwa ya mshikamano haswa baada ya kutiwa saini kwa makubaliano ya kuwa na sarafu moja. Umoja huu wa sarafu unaiweka jumuiya yetu kwenye awamu nyingine na ni hatua muhimu. Kutiwa saini kwa makubaliano Haya pia ni mwamko mpya wa mshikamanno wa kifedha."
Kutiwa saini kwa sheria hii ya sarafu moja kunatoa nafasi kwa nchi wanachama kuanza kuondoa sarafu zao za ndani ya nchi ili baadaye kuanza kutumia sarafu ya pamoja kote kwenye jumuiya ya afrika mashariki.
Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo ambaye ni Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anaiona hii kama hatua muhimu ambayo itavutia zaidi wawekezaji kwenye eneo la afrika mashariki.
"Wafanyi biashara watapata Uhuru zaidi wakufanya shughuli zao huku nao wawekeaji wakiongezeka wakipata fursa bora ya kuja kwenye kanda hii. Tukiwa na manufaa kama hayo bila shaka uwekezaji utaongezeka na kuboresha uchumi wetu"
Chini yasheria hii nchi wanachama wa EAC wanatakiwa kuwasilisha sera zao za kubadilisha fedha kwenye benki kuu ya afrika mashariki itakayobuniwa, hii ikiwa ni hatua za kuelekea kuwa na sarafu ya pamoja.
Wajibu wa benki hiyo kuu ya afrika mashariki itakuwa ni kuthibiti dhamani ya sarafu moja na pia kusimamia maswala yote ya kifedha kwenye kanda.
Lakini ingawa viongozi wa afrika mashariki wanaisifu hatua hii ya sarafu moja na kuitaja kuwa yenye manufaa kwa mshikamano, wataalam wanahoji kwamba bado kuna maswala muhimu kuliko kuwa na umoja wa sarafu kama vile biashara baina ya nchi wanachama.
Bwana Louis Kasekende ni naibu gavana wa benki kuu ya Uganda.
"Sitaki tuzingatie kupita kiasi kuwa na sarafu ya pamoja. Lazima pia tuzingatie mambo ambayo tungependa kufanikishsa Kama vile maswala ya maendeleo ya kiuchumi. Tunahitaji kufanya biashara zaidi kwa kuuza bidhaa na huduma miongoni mwetu."
Lakini Gavana wa benki kuu ya Tanzania Profesa Benno Ndulu ana maoni tofauti.
"Tutakuwa tu na sarafi moja kwa hiyo inarahisisha sana biashara na inarahisisha pia kuwa na soko moja kubwa"
Tayari jumuiya ya afrika mashriki imefanikiwa kubuni soko la pamoja na umoja wa forodha hali ambayo imeimarisha biashara kufuatia kuondolewa kwa vikwazo vya barabarani na pia mipakani.
Nchi zote tano zina zaidi ya watu million 135 na kwa pamoja zina pato la jumla la dola bilioni 85.

Mkataba huu wa sarafu moja uliotiwa saini leo utatekelezwa ndani ya miaka kumi na hapo ndipo jumuiya ya afrika mashariki itaanza kutumia pesa moja tu.

NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KUTUMIA SARAFU MOJA BAADA YA MIAKA 10

NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KUTUMIA SARAFU MOJA BAADA YA MIAKA 10
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi6HV-LW830SD6AESsqbWZBWw3W6BPQpPw-32PrjPAUbyNf6DPK3oK_hoIVvFmMoGAGC3AqmK07AtmWT84jKi2UXJmwef71-5rLiV0j3gd5UlyvA4j3vFbMigUV6J971bQagFN5sc_yWg9y/s640/MONETA.jpg
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayeshughulikia Miundombinu,Dk Enos Bukuku akizungumza na waandishi wa habari jijini Kampala leo juu ya hatua zilizofikiwa katika kuweka saini Itifaki ya Sarafu Moja jumamosi wiki kwenye Uwanja wa Kololo nchini Uganda,kushoto ni Mkufunzi na Mwandishi Mkongwe,Jenerali Ulimwengu.

Na Mwandishi Wetu,Kampala

Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jumamosi wiki wameweka saini Itifaki ya Sarafi Moja ikayowezesha matumizi ya Sarafu moja katika nchi hizo.

Matumizi ya Sarafu moja yatachukua muda kutekelezwa  ili kutoa nafasi ya utekelezaji wa michakato mbalimbali ya kuoainisha sera na sheria ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa taasisi kadhaa kabla ya kuanza kutumika Sarafu hiyo inaweza  kuchukua miaka 10.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ,Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayehusika na Miundombinu,Dk Enos Bukuku amesema utaratibu huo utazifanya nchi wanachama kukubaliana katika mambo ya sera za fedha za Jumuiya hiyo na kuwa na Benki Kuu ya EAC.

Amesema wataalamu katika Sekretariat ya Jumuiya hiyo wamekua wakienda kujifunza mfumo wa utendaji kazi wa Sarafu moja kwenye nchi za Umoja wa Ulaya(EU). 

Breaking News
Loading...

Search This Blog

LIKE PAGE ZETU ZA FACE BOOK

ZINGINE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...