MICHONGO KAMILI

Friday, 28 February 2014

WEMA AFUNGUKA KUHUSU YEYE NA DIAMOND!!

Wakati skendo kadhaa za mastaa zikiendelea kuvuma mitaani kama ile ya kuhusu Mkubwa DIAMOND kumpa mimba mwanadada fulani wa kitaa na ile ya mwana dada WEMA mwana wa SEPETU kusemekana kutoka kimapenzi na mkali wa bongo fleva anaye tamba na ngoma kama BABY na ONE ANDONLY
Blog mbali mbali kama ile ya millad ayo na website ya BONGO MOVIES vina andika kuhusu wema kufunguka kuhusu mapenzi yake kwa diamond
MCHONGO KAMILI upo hivi!!!


Mwanadada Wema Sepetu ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006 ambaye kwa sasa anaendesha kampuni yake binafsi iitwayo Endless Fame inayojishughulisha zaidi na utengenezaji wa Filamu mbalimbali.

Kupitia kipindi cha Leo tena February 28 Wema Sepetu amekubali kutaja sifa za mwanaume anayempenda kuwa na mvuto kwake,swali lililoulizwa na Watangazaji wa kipindi hicho ni kuhusu mwanaume wa sifa gani anayedhani anaweza kuolewa nae ambapo Wema alijibu “Kuolewa sio shida je huyo mwanaume nampenda,maana naweza kuja kuchumbiwa lakini nisimpende”

“Mimi nampenda Mwanaume mweusi,wanaume weupe sio kwamba sijawahi kuwa nao lakini nakuwa sina mzuka nao”.

Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Diamond amekiri kwa kusema’Kweli niko na Nasib - Diamond na nadhani muda huu kutakua na utulivu ndani yake,ule utoto tuliokua tunafanya nadhani ulikua utoto na imekua Power Couple toka mwaka 2010 kwa hiyo tuna ni miaka 4 sasa,kwa sasa tumeamua kuwa serious’.
Habari kwa Hisani ya Millard Ayo
Wema Sepetu pia kaandamana na Ant Ezekiel kwenye interview ya kipindi hicho kinachorushwa na Clouds Fm.
michongokamili.blogspot.com

Friday, 21 February 2014

BONYEZA HAPA KUANGALIA MATOKEO YA FORM FOUR 2013

 UKISHA BONYEZA LINK HAPO JUU KAMA UNATUMIA COMPUTER BONYEZA CTRL + F

ILI UPATE SEHEMU YA KUSACHI JINA LA SHULE YAKO NA KAMA UNATUMIA SIMU TAFUTA SEHEMU YAKUSACHIA INAYOPATIKANA KATIKA PAGE HIYO HIYO.........


TRAILLER YA PRINCE WILLTH
Yule mkali anaetikisa Tasnia nzima ya Bongo Movie ambae ameweza kuwapiku wakali wengine katika
Tasnia hiyo ya Movie kwa hapa nyumbani Tanzania na baadhi tu ya Filamu zake
ambazo ameshaziachia kama vile BOXEERA, EDA, RAMADHANI KAREEM, na kuweza
kufanya poa sana katika soko la hapa nyumbani na hata kimataifa pia.Na si
mwingine bali namzungumzia Ussi Hajji almaaruf kama “FEY au FEYSAL”

Mkali huyo ambaye makao makuu yake kikazi na hata
kifamilia yakiwa visiwani Zanzibar akiwa chini ya kampuni yake inayofahamika
kama Zan Effects. hivi juzi kati bllog hii ilipata fursa ya kuzungumza nae in an
Exclusive Interview iliyo endeshwa na mmoj wa waandishi wa blog hii mr.Ridhione kupitia Hits fm radio 92.5

Lakini mwanzo kabisa tulitaka kufahamu kuhusiana na
lile kosa aliloweza kulifanya katika filamu yake ya mwisho iliyoko sokoni mpaka
hivi sasa “BOXEERA”, pale ambapo alikuwa ndani ya chumba na yeye akicheza kama
verry sensitive Person “mtu mwenye hisia/machache  sana” lakini yule jamaa aliingia mule ndani
na kuchukua kitabu pasi na yeye kugundua chochote kile. Alifunguka kwa kusema
“Sisi ni wanadamu na hakuna mwanadamu mkamilifu,
tumezipokea comment za watu vizuri na tumeahidi kuzifanyia kazi kwa sababu watu
wengi sana walinipigia simu na kunambia kuwa inakuwaje wewe kama jini halaf
mtu anakuja na wewe hujahisi hata chochote?? Ni jamabo ambalo haliwezekani
kabisa. Ila ilikuwa ngumu tu kurudi tena location kutokana na mambo kadha wa
kadha. Hivyo naweza kusema kuwa tutajitahidi kuwa makini pia”

Ila alipomuuliza kuhusiana na maandalizi ya Zan
Effects kwa mwaka huu 2014 kuna nini ambacho kinakuja ama nini wanafanya maaana
ni muda mrefu sasa tangu itoke BOXEERA. Alisema kuwa kutokana na ubora wa
kazi zao ambao huambatana na maandalizi mazuri ambayo lazima yachukue muda
kidogo ………

“Ila soon tyu nitaitambulish The Exclusive one ambayo inakwenda kwa jina la PRINCE WILTH ambayo itatoka katika miezi hii hii

ya hapa mwanzoni. Ijapo katika mwaka huu wa 2014 kuna movie nyingi tu kutokea
Zan Effects  ambazo zitatoka ila hiyo
Prince Wilth itakuwa ya mwanzo as an exclusive. Na naweza kusema kuwa hizi ni
movie ambazo zinaleta mapinduzi katika tasnia ya filamu ambapo ndipo kama
tulivyoanza na Boxeera kama walivyoiona. Lakini mi naahidi itakapotoka nahii
Prince Wilth ndipo watakaposaidiki hili”

Jamaa tulipotaka uthibitisho wa hayo mapinduzi kwa
movie hiyo ya Prince Wilth akatutupia kitu cha trailer ya movie hiyo na
kuifanya blog hii kuwa na sababu mia moja za kuandika habari hii yenye ushahi wakutosha.Ila jamaa alimalizia kwa kusema;
“So mi nitaendelea kufanya vitu vitakavyoleta tofauti
katika tasnia ya filamu, na ningeomba sana watu wangu waendelee kuni support
na kazi zangu ili tuweze kufikia pale ambapo tunafikiria kufika.Nawapenda sana
fans wangu wooooooooote” 
huo ndio mchongo kamili kutoka 
www.michongokamili.blogspot.com

OKWI RUKSA KUCHEZA YANGA - FIFA.


HATIMAYE Shirikisho la Soka Duniani, FIFA limemuidhinisha mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi kuichezea klabu ya Yanga. Kwa mujibu maelezo wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini, TFF, Celesine Mwesigwa amethibitisha kuwa tayari wameshapokea barua kutoka FIFA ikiwahabalisha kuwa mchezaji huyo ni halali kukipiga Yanga. Mwesingwa amesema suala Okwi tayari limeshamalizika ila hawezi kulizungumzia zaidi kwasababu watatuma taarifa kwa vyombo vya habari kwa ufafanuzi zaidi. Januari 22 mwaka huu ikiwa ni siku mbili tu kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ilisimamisha usajili wa Okwi kuitumikia Yanga ili kwanza upatikane ufafanuzi kutoka FIFA juu ya uhalali wake kucheza timu hiyo. Kamati hiyo ilifikia iliamua hivyo kwasababu ya mgogoro wa mchezaji huyo na klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia ambapo kulikuwa na taarifa kuwa alipewa kibali cha muda kuichezea SC Villa ya nchini kwao ili kulinda kiwango chake.

TOP C AFUNGUKA KUHU KUPOROMOKA KWAKE KIMUZIKI



TOP C KATIKA POUZI


Yule mshkaji ambaye alijitahidi kufanya poa sana katika Industry ya Bongo Fleva kwa hits songs zake kadhaa ikiwemo "Sababu ya Ulofa" na nyinginezo zikiwa zime recordiwa ndani ya Sharobaro Records chini yake Raisi wa Masharobaro Bob Juniour.
Nadhani kwa  intro hiyo si mgeni saaana katika masikio na macho ya mafuns  wa Bongo Fleva a.
 He is Top C ambaye kiukweli alipotea muda mrefu sana katika gemu na kufikia hata kusababisha kuwepo kwa uvumi wa kuwa jamaa alibahatisha!!! au ndo keshapigwa chini??? na vitu kama hizo nini..............!!!

TOP C
Ila  juzi kati Top c alifunguka na kuuzima ukimya wote uliokuwepo dhidi yake na kukanusha suala la kushushwa kimziki na aliyekuwa bosi wake wa zamani (Babuu Kisouji) alipokuwa chini ya Babuu Entertainment na Top C kusema kuwa.
"hapana hilo suala si la kweli, ila tu unajua sisi ni binadamu tunakosea na tunakwazana vilevile. Kuna mambo tu ya kibinadamu yaliyotokea kati yangu na bosi wangu wa zamani Babuu Kisouji na hivyo hatukufikia mwisho mzuri ndiyo maana tukaamua kila mmoja afanye shughuli zake. Ila si kweli kwamba yeye ndiyo kanishusha au kanizuia nisitoe nyimbo mpya"
Lakini pia Top C alinieleza kuwa alikuwa na baadhi ya mambo ya kifamilia na nini ndiyo maana akawa kimya, ila hivi sasa ameshajipanga vizuri na kazi yake mpya ipo tayari na hivi karibuni tyu itaanza  kusikika kwenye radio stations mbalimbali.

TOP C NA MAANDALIZI YA KITU KIPYA YAKO HIVIIIIIIIIIIIII
"Kuna baadhi ya vityu tyu vinamaliziwa na muda mfupi tyu itaanza kusikika katika redio stations mbalimbali. Sijajua ni lini hasaa itakuwa kwa hewa kutokana na hayo ni masuala ya management yangu ambayo hivi sasa inanisimamia kazi zangu kutokea kule Kenya "Canden Kane " Ila ikishakuwa tayari tyu nitaitambulisha"
Na zaidi ya hayo Top C anawaomba mashabiki wake mumpokee vizuri na mumpe support ya kutosha.

Wednesday, 19 February 2014

"HIVI SASA NI WAKATI WA KUTENGENEZA IMAGE YA JERUSALEM PEKEE".................... ASEMA JACOB STEVEN

YULE MKALI WA SHKAMOO MZEE NA NYINGINE NYIIINGI YAANI "JB" JACOB STEVENANAKUJA NA CHUMA KINGINE "WAGENI WANGU"

TRAILLER YA WAGENI WANGU

Utakapozungumzia watengenezaji wazuri wa
filamu za Kitanzania huwezi kuacha kuwataja Jerusalem
Film ambayo kampuni hii ipo chini yake Bonge la Bwana “JACOB STEVEN” ambaye pia
katika waigizaji wanaofanya poa sana
hivi sasa katika soko la filamu ndani na nje ya nchi pia huwezi kuacha

kumuorodhesha huyu jamaa.

JB KATIKA POUZI
Juzi kati tulipata fursa ya kuzungumza
nae na tukataka kufahamu mengi sana kutoka kwake
lakini pia kutokea Jerusalem Film akiwa kama mzungumzaji mkuu wa Kampuni hiyo. Na kitu cha mwanzo
kabisa tulichotaka kufahamu ni kuhusiana na suala zima la Jerusalem kutoa
filamu ambazo JB hatujamuona humo ndani hata scene moja, jambo ambalo
limewaumiza vichwa mashabiki wake wengi katika filamu iliyokwenda kwa jina la
BADO NATAFUTA.
alikuwa na haya yakusema;
“Yeah ni kweli, ila lengo la kufanya
hivyo ni kutaka kutengeneza image ya kampuni ya Jerusalem
Film na si lazima ya JB, kwa maana ya kuwa watu wawe na hamu ya kutazama filamu
za Jerusalem. Na
huo naweza nikasema ndiyo mpango wa hivi sasa kwa maana ya kuwa kutakuwa na
filamu za aina mbili ambazo nitakuwa sishiriki na zile ambazo nitakuwa
nashiriki”.
OFFICIAL COVER YA MOVIE AMBAYO IMEFANYA POA SANA 2013 "BADO NATAFUTA"
Lakini jambo jengine ambalo JB
alilizungumzia ni kwamba anawashukuru sana mashabiki wake kwani filamu hiyo ya
BADO NATAFUTA imekuwa filamu ambayo imefanya vizuri sana mwaka jana.Ila bado
tukawa na maswali kwa JB kuwa kwanini ameamua kuhamia katika kutengeneza image

ya Kampuni tu na si JB kama JB?
 
Bi Staa kama anavyojulikana na wengi....
“Hapana, ila unajua jambo muhimu ambalo
tumelilenga hapo ni kuwafanya mashabiki wakishakuwa na imani na Jerusalem ijapo
kuwa JB hayumo ndani ya filamu hiyo itasaidia sana pale ambapo nitakuwa siigizi
tena kutokana na sababu mbalimbali huwenda nimeamua kupumzika, au kwa sababu
nyengine yeyote ile. Hivyo watu bado watakuwa na imani na vitu vinavyozalishwa
na Jerusalem.”
GABO AKIWA KAZINI
Na jambo jengine ni kuhusiana na
mipangilio ya Jerusalem kwa mwaka huu 2014, maana tayari ni mwezi wa pili huu
hivi sasa tunaelekea na hatujaona wala kusikia kazi yeyote mpya kutokea kwako.
Suala ambalo alinieleza kuwa wapo vyumbani wakikamilisha mapishi ya kazi mpya nyiingi
tu ambazo soon zitakuwa sokoni.
GABO AKIWA KAZINI ALIYEKUWA MAIN CHARACTER NDANI YA BADO NATAFUTA
“Kwa filamu ambzo mimi sishiriki mwaka
huu tutakuwa na filamu itakayoitwa WAGENI WANGU ambayo ameshiriki Bi
Hindu,Mhogo Mchungu,Bi Star, na  mzee
mwingine wa Mombasa ambayo hii itatoka recently, halafu tutakuwa na POLICE LOCK
UP ambayo atakuwepo Ben Kinyaiya,Brigit (ambaye ameigiza kama Regina) na Adam
Kuambiana, then tutakuwa na filamu nyingine inaitwa  CHA USIKU ambayo wameshiriki Mayasa Mrisho,
Hemed Suleiman,Cathy Rupia, Shamsa Ford, Brigity na Baba wa Hisia “Haji Adam.
Ila kwa upande wa movie ambazo nashiriki ya kwanza kabisa itakuwa ni HUKUMU YA
NDOA YANGU ambayo nimecheza na muigizaji wa siku nyingi sana Chiki Mchoma,
Mayasa Mrisho, Shamsa Ford, Bi Mwenda, Q Chief, Brigity na Will Sanga. Ambapo
nafikiri movie hii itatoka mwezi wa tatu ama nne”
 
Katika malengo mazuri kabisa ya JB kwa
kutengeneza image ya kampuni yake ni pamoja na suala zima la kuwapa nafasi  au kuwafungulia milango waigizaji mbalimbali
wadogo ili kuwapa nafasi na kuwa waigizaji wakubwa na waigizaji wapende kuigiza
Jerusalem
either JB yupo ama hayupo. Sasa suali langu lilikuja likiuliza kuwa je ni
kuibua  vipaji au vipi maana kama ni kuibua vipaji hatujaona katika mfululizo huo
alionitajia jina ambalo ni jipya katika masikio yetu lakini pia hata katika

movie ya Bado Natafuta halikadhalika.
GABO KATIKA POUZI
“Swali zuri sana, Jerualem haibui vipaji
ila ni inaendeleza vipaji maana kuibua vipaji ni risk. Maana wapo waigizaji
waliokwisha anza kuigiza na wana vipaji, hivyo sera yetu ni kuwapa nafasi

waigizaji hao na kuwafanya wawe waigizaji wakubwa kwa kuwapa movie nyingi.”
JB AKIFURAHIA KAZI NZURI WALIYOIFANYA ZANZIBAR BAADA YA KUTWAA KITU HICHO (KOMBE0
Baada ya maongezi mengi sana na Bonge la Bwana “JB” kupitia 92.5 Hits
fm radio ikishirikiana na Www.ridhiwanshariff.blogspot.com,
kabla ya kumpa nafasi ya kuzungumza na fans wake ikanibidi na mie nimpatie

hongera yake kwa movie ya BADO NATAFUTA kwani hata mie imenivutia.
JB KATIKA POUZI YA PICHA NA JEZI YA TANZANIA
“Thanks bro, Nawaahidi kuwa movie ambazo
tumezitengeneza mwaka huu 2014 watazipenda sana maana waigizaji hawa waliocheza nimekaa
nao kwa muda mrefu tumefundishana, tumeelekezana na kila mmoja ameonesha ana
uwezo mkubwa. Hivyo nawaahidi kwamba hata movie ambazo sitashiriki watazipenda
sana kama ambazo nimeshiriki na mfano wameshaanza kuona kwa BADO NATAFUTA ni
filamu ambayo imefanya vizuri sana na hata zile ambazo nimeshiriki zingine

hazikupendwa sana kama hii ambayo sijashiriki”.


KUPITIA HAPA
HAPA Www.Michongokamili.com UTAWEZA KUSIKIA INTERVIEW YA
JACOB STEVEN NA RIDHIONE SHARIF WA ZANZIBAR
JACOB NA IRENE  KAZINI
Breaking News
Loading...

Search This Blog

LIKE PAGE ZETU ZA FACE BOOK

ZINGINE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...