Ni wakati mechi kati ya yanga na al ahly ya egypt ikiendelea mida ya saa 2:30 usiku wa jumapili hii ambapo gari aina ya FUNCARGO yenye plate number T763 AXJ ikiendeshwa na mwanamama ambaye jina lake halikupatikana ilipogonga ukuta wa nyumba iliyopo karibu na ZAHANATI ya kiserekali ya segerea ugombolwa kwa maelezo ya walioshuhudia ajari hiyo inasemekana mama huyo alikuwa amelewa kiasi flani na alikuwa akitokea barabara ya inayo toka shule ya msingi segerea na alipo fika karibu na kona iliyopo kwenye zahanati hiyo alitakiwa akate ili kuelekea barabara ambayo ingempeleka moja kwa moja hadi kituo cha mabasi cha kwa bibi, ndipo hapo alipo kosea badala ya kukanyaga break akajikuta anaongeza spidi na kugonga nyumba iliyopo mbele yake ambayo ni ya bwana mmoja aliye julikana kwa jina la Mr. Msofe. dakika tano baada ya ajari hiyo watu wengi walijaa eneo la tukio akiwemo Mr. Msofe ambaye ni mmiliki wa nyumba hiyo,alipo jaribu kuhojiwa mama huyo ilishindikana kwani alionekana amechanganyikiwa na asingeweza kutoa maelezo yoyote yakueleweka kwa muda huo na pia alikuwa akilalamika kupatwa na maumivu maeneo ya kichwani..
MICHONGOKAMILI.BLOGSPOT.COM
No comments:
Post a Comment
0653830825