MICHONGO KAMILI

Friday 21 February 2014

OKWI RUKSA KUCHEZA YANGA - FIFA.


HATIMAYE Shirikisho la Soka Duniani, FIFA limemuidhinisha mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi kuichezea klabu ya Yanga. Kwa mujibu maelezo wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini, TFF, Celesine Mwesigwa amethibitisha kuwa tayari wameshapokea barua kutoka FIFA ikiwahabalisha kuwa mchezaji huyo ni halali kukipiga Yanga. Mwesingwa amesema suala Okwi tayari limeshamalizika ila hawezi kulizungumzia zaidi kwasababu watatuma taarifa kwa vyombo vya habari kwa ufafanuzi zaidi. Januari 22 mwaka huu ikiwa ni siku mbili tu kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ilisimamisha usajili wa Okwi kuitumikia Yanga ili kwanza upatikane ufafanuzi kutoka FIFA juu ya uhalali wake kucheza timu hiyo. Kamati hiyo ilifikia iliamua hivyo kwasababu ya mgogoro wa mchezaji huyo na klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia ambapo kulikuwa na taarifa kuwa alipewa kibali cha muda kuichezea SC Villa ya nchini kwao ili kulinda kiwango chake.

No comments:

Post a Comment

0653830825

Breaking News
Loading...

Search This Blog

LIKE PAGE ZETU ZA FACE BOOK

ZINGINE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...