MICHONGO KAMILI

Saturday 26 April 2014

SHEREHE ZA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZAFANA.




Sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizo fanyika katika uwanja wa zamani wa taifa zimefana sana kwa halaiki na maonyesho ya kijeshi yaliyofanywa kuanzia asubuhi hadi mchana huku mgeni rasmi akiwa raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, sherehe hizo zimefanyika huku mwenyekiti wa bunge maalum la katiba akiwa ameahirisha shughuri za bunge hilo ili kupisha bunge la kujadili bajet liendelee na shughuli hiyo hadi mwezi wa nane ndio bunge maalum la katiba litaendelea.

Tuesday 22 April 2014

HATIMAYA MOYESA ATUPIWA VIRAGO

 

Mkufunzi mkuu na meneja wa klabu ya Manchester United David Moyes ametimuliwa.

David Moyes amefutwa kazi baada ya kushikilia usukuni wa klabu hiyo kwa miezi kumi tu.

Moyes, mwenye umri wa miaka 50, aliteuliwa na Ferguson kumrithi alipostaafu mwaka jana baada ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.

Taarifa kutoka kwa klabu hiyo imemshukuru Moyes kwa bidii, uaminifu na hekima aliyoonyesha kocha huyo akiwa mkufunzi wa Manchester United.

Moyes alichukuwa usukani wa kuifunza Manchester United mwaka uliopita baada ya aliyekuwa kocha wa siku nyingi Sir. Alex Ferguson kustaafu.

Huku zikiwa zimesalia mechi nne pekee msimu wa ligi kukamilika Mancheseter united inashikilia nafasi ya saba kwenye jedwali la msimamo wa ligi hiyo alama ishirini na tatu nyuma ya viongozi Liverpool.

Klabu hiyo imeshindwa kufuzu kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takriban miaka ishirini.

NI KIJANA MWENYE UMRI USIO ZIDI MIAKA 25 ALIYE SOMA ALFAROUQ SEMINARY AKAENDA LIDA BOYS ILIYOPO LINDI NA SASA YUPO CHUO FLANI FLANI HIVI AKIWA NA KIPAJI CHA AJABUUUU ALIANZIA KUPAZA SAUTI CHINI YA MITI ALIPO KUWA LIDA BOYS LAKINI ALIPO FIKA CHUO ALIKUTANA NA PRODUCER AITWAE CHRISS NA AKAMPA NAFASI YA KUPAZA SAUTI MBELE YA KIPAZA NA HII NGOMA HAPO CHINI NDICHO KILICHOJIRI.............PERFECT FOR BEGGINER! NAIDEDIKET HII KWA WAPENZI WA BLOG HII .....I MISS YOU SO MUCH



Sunday 13 April 2014

ALAZWE MAALI PEMA PEPONI REJENDARI MAALIM GURUMO




inna lilah wainna ilaih rajiun...Ni mzee wa siku nyingi sana kwenye
muziki Tanzania ambae aliwahi
kuingia kwenye vichwa vya habari
mara nyingi hasa kutokana na
kuugua kwake kuliko mfanya asitaafu
kabla ya kuzawadiwa gari na
mwanamziki wa kizazi kipya
“Nasibu” au Diamond
Taarifa zilizothibitishwa na hospitali
ya Taifa Muhimbili  zimesema Mzee huyu
amefariki dunia akiwa hospitalini
hapo leo April 13 2014 saa nane
mchana baada ya kupelekwa  jana
asubuhi na kulazwa kwenye wodi
namba 6 ya Mwaisela kutokana na
kuzidiwa.
Tayari mwili wake umepelekwa
kwenye chumba cha kuhifadhia maiti
msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata makuburi
na mimbango ya mazishi itafanyika hapo.
Blog hii inatoa pole kwa wafiwa wote na
wapenzi wa muziki mzuri uliokuwa ukifanywa na
mzee wetu Maalim gurumo
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA
PEPONI ROHO YA MAREHEMU
MAALIM GURUMO
“AMIN"

Friday 4 April 2014

HII NDIO HOTUBA YA RAIS KIKWETE BUNGE LA KATIBA MARCH 21 2014 BUNGENI DODOMA

Kwanza kabisa nianze kwa kuwaomba radhi kwa kuchelewa kuwawekea kitu muhimu kama hichi, hii ni hotuba ya muheshiwa rais JK akihutubia bunge maalum la katiba mjini dodoma mwezi march tarehe 21  2014 . unaweza kudownload  audio  yake  hata video yake pia ilikuweza kufuatilia kilichoendelea siku hiyo....nime fanya hivi ili kuwapa wasomaji wangu nafasi ya kuwa na audio ya hotuba hii kwaajili ya kufuatilia zaidi juu ya kinachoendelea mjini dodoma...




 

MICHONGOKAMILI.BLOGSPOT.COM

KATANGAZEEE NI HII HAPAAA (DOWNLOAD HAPA)


Wednesday 2 April 2014

TRENI YA MWAKYEMBE INATUTIA MASHAKA!!!!

 

 Ni kama mwaka mmoja na nusu sasa toka treni ya shirika la reli la tanzania (TRL) ianze kufanya safari zake za kusafilisha abiria kupitia maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam, treni hii imekuwa msaada mkubwa kwa watu wanao tokea maeneo yenye idadi kubwa ya wakazi wa jiji hili ambamo treni hiyo imekuwa ikipiga ruti zake za kila siku ukiacha mbagara, kama wewe ni mmoja wa watumia wazuri wa treni hiyo utakuwa umeshuhudia idadi kubwa ya watu wanaotumia usafiri na kupunguza foleni kubwa zilizokuwa zikitokea maeneo ya posta,kariakoo na buguruni


treni hii imekuwa ikikumbwa na matatizo kadhaa ambayo kwa jicho la pili yanaonekana yanazuilika kama ilivyo pata ajari ya kugongwa na roli lenye namba za usajili T 124 ATG   mnamo tarehe 03 October mwaka 2013 lakini tatizo hili lisingewezakutokea kama askari wa barabarani wange tumika maeneo ambayo treni hiyo inapita ikikatiza katika barabara mama za jiji zinazo pitisha magari kwa wingi zaidi kama ile ya buguruni,tabata na ubungo, lakini kikubwa kilicho igusa blog hii hadi kuandika juu ya usafiri huu ni usumbufu uliotokea siku mbili mfululizo kati ya tarehe 1 hadi 2 ya mwezi wa 4 mwaka huu 2014, tarehe 1 mida ya usiku wa saa mbili treni hiyo ilitakiwa imalizie safari yake ya mwisho kutoka stesheni hadi ubungo, abiria wake walikata tiketi kama kawida na kuingia kwenye treni hiyo tayari kwa kysafiri lakini ilipofika saa 2 na dakika kama 20 hivi ilitangazwa kuwa treni hiyo haitoweza kumalizia safari hiyo na abiria wanaombwa radhi kwa usumbufu huo, tatizo kubwa lililotajwa ilikuwa kufeli kwa injini zinazo sukuma gari moshi hilo lakini ilipofika tarehe mbili tena mwandishi wa blog hii alifika katika stesheni hiyo ili kujua kama treni hiyo imeanza safari zake au la! lakini alikuta milango ya ofisi hizo imefungwa na hakuna tangazo lolote lililowekwa kuwataarifu abiria wa usafiri huo ambao jana yake walikatishwa tiketi na hawakurudishiwa pesa zao kwa madhumuni ya kutumia usafiri huo kesho yake yaani tarehe 2 . hivi ni kweli TRL inakosa pesa ya kufanya matengenezo ya injini za treni hizo? kwa mahesabu ya haraka haraka kama kila abiria mmoja analipia shs 400 kwa safari moja na treni ni hiyo kwa kadilio la chini ina uwezo wa kuchukua takribani abiria 1000, hii inaleta jumla ya shs 400000 kwa safari moja tu! chakujiuliza ni  je kwa siku inafanya safari ngapi? na inaingiza shilingi ngapi? na ina muda gani toka ianze! hadi shirika hilo likose pesa ya kufanya marekebisho ya injini hizo?. mi sina mengi yakunena! ni hayo tu!!!
MICHONGOKAMILI.BLOGSPOT.COM
Breaking News
Loading...

Search This Blog

LIKE PAGE ZETU ZA FACE BOOK

ZINGINE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...