MICHONGO KAMILI

Wednesday 21 January 2015

TIMU NNE ZA ULAYA ZINAWANIA SAINI YA MSHAMBULIAJI MBWANA ALLY SAMATTA

Kwa namna moja au nyingine Huenda uukawa ni mwaka wa neema kwa mshambuliaji Mbwana Samatta wa TP Mazembe kwa kuwa timu nne za Ulaya zimeonyesha nia ya kumchukua.
http://soka360tz.files.wordpress.com/2013/07/capture-20130627-082245.png
Habari za chinichini kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje zinachombeza  kuwa, timu nne zimeanza mchakato wa kuwania saini ya mkali wa TP Mazembe SAMATTA, kati ya hizo ambazo ni kutoka katika nchi za Ufaransa na Italia, zimeonyesha nia ya kufanya kazi na mshambuliaji huyo Mtanzania.
“Kweli tunayajua majina ya timu nne, kumekuwa na mawasiliano kupitia meneja wake Tanzania pamoja na uongozi wa TP Mazembe,” kilieleza chanzo kutoka Ufaransa.
“Tusingependa kuanza kueleza kila kilichopo kwa sasa wala kuzitaja timu zenyewe, lakini tunaamini Samatta anaondoka Mazembe msimu huu.” Alisema tajiri wa TP Mazembe Billionea  KATUMBI.
Baada ya taarifa hizo, juhudi zilifanywa na baadhi ya social media ili kumpata meneja wake, Jamal Kisongo ambaye alitoa ushirikiano.
“Kweli kuna timu zinamhitaji, kama nilivyokueleza awali Mbwana si mtu wa kwenda kufanya majaribio, badala yake kujiunga na timu na kuanza kazi.
“Sasa kinachofanyika ni taratibu na nimekuwa na mawasiliano na uongozi wa TP Mazembe, hivyo vuteni subira kidogo,” alisema Kisongo akionyesha kujiamini kuhusiana na mchezaji wake huyo.
Samatta yupo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko na amekuwa mchezaji tegemeo wa kikosi cha Mazembe.
Awali ilielezwa, mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi, alikuwa akifanya juhudi kuhakikisha Samatta anabaki Lubumbashi, DR Congo, lakini Kisongo amehakikisha anakwenda mbele zaidi ili kupata mafanikio zaidi.

No comments:

Post a Comment

0653830825

Breaking News
Loading...

Search This Blog

LIKE PAGE ZETU ZA FACE BOOK

ZINGINE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...