MICHONGO KAMILI

Saturday 6 December 2014

STEVE R&B ALALAMIKA KUIBIWA NYIMBO NA UNDERGROUNG WANAOISUMBUA MIKOA KWA SASA.

 
Wakati macho na masikio ya Watanzania wengi kwa siku kadhaa yalielekezwa Dodoma katika mjadala uliokuwa ukihusiana na suala la wizi wa fedha zaidi ya shilingi bilioni 320 katika akaunti ya Escrow Tegeta,kwa upande wa burudani nako suala la wasanii kuendelea kulizana katika kazi zao limeendelea kushika kasi ya ajabu hali ambayo inaweza kusababisha mitafaruku mikubwa kati yao.

Hivi karibuni msanii chipukizi ajulikanaye kama  Alawi Abdallah akitumia jina la kisanii ambalo ni  Decent Boy (A5) akiwa na Joseph Msunyalo almaarufu kama Jos Joh waliachia singo yao inayojulikana kwa jina la X-Girlfriend ambayo walidai kwamba wamemshirikisha Steve RNB  na ilisambazwa katika vituo mbalimbali vya redio na blogs mbalimbali ikiwemo Hassbaby Mapacha ,Funguka Live na Bongo Swaggz lakini katika hali ya kushangaza kumekuwa na uvumi unaoeleza kuwa Steve RNB amedai kuibiwa ngoma yake hiyo aliyokuwa ameicha studio ikiwa bado haijakamilika.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka katika chanzo chetu cha habari cha blog flani hapa town kimeeleza kuwa Steve RNB,alidai kwamba ngoma hiyo alikuwa akiifanya katika studio ya Chief Elia ambayo inapatikana maeneo ya Sinza na alikuwa ameitunga maalum kwaajili ya mpenzi wake lakini anashanga kuiisikia kupitia vyombo mbalimbali vya habari huku ikidaiwa kwamba ameshirikishwa ilhali wimbo huo ni mali yake.

Katika kutaka kuujua ukweli niliwatafuta Decent Boy naJos Joh ambao wapo mkoani Kilimanjaro kimasomo kwa sasa walieleza kuwa wimbo huo waliufanya kwa kumshirikisha Steve RNB na hakuna ukweli wowote kuhusiana na hilo.
“Ukweli ni kwamba wimbo huo tuliufanya kwa kumshirikisha Steve na wala haukuibwa kama ambavyo watu wengi wamekuwa wakidai na mimi binafsi nimesikitishwa kusikia hivyo kwani toka nilipoanza kufanya shughuli zangu za muziki sijawahi kufikiria kufanya hivyo.

Aidha Decent boy ambaye amewahi kufanya nyimbo kama Stress akiwa na Jos Joh pamoja na Lazima ukae, amesema kuwa anatarajia kuachia ngoma mpya itakayokwenda kwa jina la “Kilaza” akiwa amemshirikisha Ali Nipishe, na pia Jos Joh  kuachia wimbo wake unaojulikana kama “Sitokusahau” akimshiriksha mwanadada Ayler ambapo nyimbo zote zimefanyika  katika Studio ya Kili Records chini ya Producer Rash the Don.

Hii si mara ya kwanza kwa wasanii nchini kukumbwa na kashfa ya kuibiana kazi zao na miongoni mwa wasanii waliowahi kukukmbwa na kashfa hizo ni pamoja na Diamond aliyewahi kudaiwa kuiba wimbo wa My number one,TID wimbo wa Nyota Yangu na Ben Paul aliyedaiwa kunakili wimbo wa Jikubali.

No comments:

Post a Comment

0653830825

Breaking News
Loading...

Search This Blog

LIKE PAGE ZETU ZA FACE BOOK

ZINGINE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...