TANGAZO
MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA
JESHI LA KUJENGA TAIFA LINAPENDA KUWATAARIFU
VIJANA WATAKAOHITIMU KIDATO CHA SITA MEI 2015,
KUWA WATAJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA
MUJIBU WA SHERIA KUANZIA JUNI 2015. ORODHA YAO
NA VIKOSI WATAKAVYOPANGIWA ITATOLEWA BAADA
YA MAWASILIANO KUKAMILISHWA KATI YA JKT NA
BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA - NECTA.
AIDHA, JKT LINATOA UFAFANUZI KUWA, MAFUNZO YA
JKT YALIYOAHIRISHWA NI KWA WALIMU NGAZI YA
CHETI NA DIPLOMA WALIOKUWA WAJIUNGE NA
MAFUNZO HAYO MWEZI JANUARI HADI MACHI 2015.
MAFUNZO YA JKT HAYAKUSITISHWA KAMA
ILIVYOANDIKWA KWENYE BAADHI YA VYOMBO VYA
HABARI PAMOJA NA MITANDAO YA KIJAMII.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MAKAO MAKUU YA JESHI LA
KUJENGA TAIFA.